MISTARI YA WIMBO HUU

Mhm mhm
Ujana ni maji ya moto
Yashaniunguza mi nataketea
Niliwakana watoto wangeniuguza sikutegemea
Na kama dunia tambala langu lishatoboka
Sina hata pa kulala nakesha kwa Kimboka
Wale marafiki niliokula nao
Na kunisifu sasa siwaoni
Eti sina kiki siendani nao kwa kuwa sina kitu mfukoni

Kama pesa nilipata nikadharau hadi wazazi
Nikakesha kula bata najisahau
Na kumwaga radhi

Ohh sina (ooh yani sina)
Ohh sina (wa kunipa imani)
Ohh sina (ooooh sina mama)
Oooh sina
Iyeyeee
Ohh sina (hata wa kunifariji)
Ohh sina (kunipa moyo niendelee)
Oooh sina (Oooh sina mama)
Ohhh sina
Oooiyee

Mhm
Asiyefunzwa na mama hufunzwa na dunia
Misemo ya wahenga
Family ndugu lawama
Sikutaka karibia kwangu
Nipokee
Ponda mali eti kufa kwaja
(Heheheeee)
Kumbe nivukako mbali navunja daraja
Jua likizama nafsi nanyongea mawazo
Nani nimpe lawama
Peke yangu naongea hamnazo

Kama pesa nilipata nikadharau hadi wazazi
Nikakesha kula bata najisahau
Napumua karadhi

Ohh sina (ooh yani sina)
Ohh sina (wa kunipa imani)
Ohh sina (ooh sina)
Oooh sina
Iyeyeee
Ohh sina (hata wa kunifariji)
Ohh sina (kunipa moyo niendelee)
Oooh sina (ooh sina mama)
Ohhh sina
Oooiyee

Pesa pesa
Pesa Pesa
Pesa Pesa
Pesa pesa
Pesa pesa
Pesa mfano wa poto (pesa pesa)
Zinapepea sare ndo sindano (pesa pesa)
Chunga yasije majuto (pesa pesa)
Tena tekea igeni mifano

Toa Maoni Hapa

SHIRIKISHA MWINGINE

Your email address will not be published. Required fields are marked *

SHIRIKI KUONGEZA MISTARI

VIDEO YA WIMBO HUU