MISTARI YA WIMBO HUU

Bamboohh
Fantente vakuntazani

Nilipotoka mbali na ninaheshimu nilipo
Sikuwa na umuhimu kihivyo
Stimu zikanipa elimu ya Biko
Kimaandiko kimistari hadi fans wanascream nikirap
Sikuamini kama nina zari mpaka nilipoi-dream HipHop
Wanapagawa na baadhi ya mambo nayoyajua
Pia nina uwezo wa kufanya mpaka madawa yanaugua
Wanapagawa na nyimbo ngumu hawa team mabiitoz
Achana na power window sijui rimz za Dimpoz
Haileti bingo mshiko star ishi simple
Sanaa iko hivyo sometimes hukataa kukaaa ulipo
Wanaodharau hujiletea matatizo hawajui kama wadau hupendelea kukuona hivyo
Bonge la staa donge la njaa hauna kitu
Jikombe ugongwe mtaa ukuone hauna ishu
Ukishindwa kujiandaa jiandae kushindwa
Mjinga utaachwa unashangaa kumuona Martin Kadinda
Usmati anaotinga majumba mandinga ya bwana Almasi
Je hizi tracks za harakati ni ujinga
Hapana nguvu ya mamba ni maji
Na umaarufu au kutamba kushika namba ni bahati
Sio kipaji kama Kubanda eti unachana kigumu
Kisa track ikivuma sana kwenye chati haidumu
Amani kwa chachage na makuwadi wa soko huria
Baba asante kwa utafiti na zawadi ya almasi ya bandia
Nyumbani nasikiliza Dunia Ya Sasa ya Marijani
Najiuliza tutarithi nini ikiwa imani ishakwisha tangu zamani
Labda kubisha na wakinitisha najihami
Inasikitisha unapoibiwa na aliyekupigisha ni jirani
Pole Maprossoo uhujumu uchumi umefanya umetubu
Wazee ni wahuni hadi soo waay back before Sugu
Taifa la kondoo huendeshwa na serikali ya Dubu
Na mbwa mwitu wenye siri ili bepariumuabudu
Kimahakama kiserikali kidini umsujudu
Huo ni utumwa pia unafanya vijanawanaumia
Tunaishia kufia mabatani kama nzi ndani ya glass ya bia (bia)

Siri ya mtungi aijuaye kata
Komaa kaza kisha utapata
Siri ya mtungi aijuaye kata
Komaa kaza kisha utapata
Siri ya mchezo naijua mimi tu na hakuna mwingine
Siri ya mchezo naijua mimi tu na hakuna mwingine

Tofauti ya biashara na siasa
Ikila hasara inaweza buma
Wakati siasa kila mara ukiwa unang’ara ujue kuna kinara
Anayeunda msafara wa wanaojituma
Na kuchuma kwa kukufanya uwe imara hapo hasara
Hakuna Kidumu Chama Cha Masela (kidumu)
Ukoloni mambo-leo umetupa uhuru wa bendera
Tuone kufuru za wenye hela
Tanzania ni demu wa mtungo wanamuiita cha wote
Hangover anaikimbia kwa kupiga mtungi saa zote
Mkubwa anazuga ata-solve matatizo ya nchi yake
Na gari bovu halisukumwi kwa kukaa ndani yake
Maendeleo ni ile ndoto mwekezaji ashaipuuza
Je kukaa karibu na moto ni kuuota au kujiunguza
Hakuna uhuru wa kweli (Afrika) msidanganywe na illusion
Na daily tunafeli sababu ya political institutions
Civilization ime-advance sasa wanatuua economically
Hakuna utumwa mbaya kama ule wa kujiona uko free
Kuusaka ukweli ni sawa na kumenya kitunguu
Kila ganda litakutoa machozi na utabaki macho juu
Ukishafika kwenye kiini niambie nini utagundua
Zaidi ya mafaili yaliyounganika utaghairi kuyafunua
Wamejivisha unoah safina zao zikatoboka
Wakajivisha umussa fimbo zao hazikugeuka nyoka
Sasa wanaujaribu umungu mtu kuamua nani leo atatoka

Siri ya mtungi aijuaye kata
Komaa kaza kisha utapata
Siri ya mtungi aijuaye kata
Komaa kaza kisha utapata
Siri ya mchezo naijua mimi tu na hakuna mwingine
Siri ya mchezo naijua mimi tu na hakuna mwingine

Kunuli
Tz Tanzania
Fid Sir
Wakunuli kutuli kunava
Hiki ni kimwana cha Kitanzaniano
Foma mwintu nontena daji baba

Toa Maoni Hapa

SHIRIKISHA MWINGINE

Your email address will not be published. Required fields are marked *

SHIRIKI KUONGEZA MISTARI

VIDEO YA WIMBO HUU