MISTARI YA WIMBO HUU

Eeh siri ya penzi uvumilivu
Ukiwa na hali we utaaribu
Haki yake mtendee, akikosa msamehe
Yakipita yamepita mgange yajayo
Eeh siri ya penzi iih kuheshimiana
Achana na jeuri, achana na kiburi
Siri zake mlindie, mali zake mtunzie
Hadharani chumbani, mthamini mwenzio

Ngoja nikwambie eh ili umwambie, nikwambie
Ngoja nikwambie ee eh nikwambie umwambie
Ngoja nikwambie eh ili umwambie, nikwambie
Ngoja nikwambie ee eh nikwambie umwambie

Ukishikwa masikio na wasiokutakia mema we utapotea (aah haa)
Maneno ya nje sumu, sio kila jirani mwema
Kuwa makini (aah haa aahaa)
Siri ya penzi (ou ohh ohoo)
Kutofichana (aah haa aahaa)
Siri ya penzi (ou ohh ohoo)
Kuaminiana

Ngoja nikwambie eh ili umwambie, nikwambie
Ngoja nikwambie ee eh nikwambie kwambie
Ngoja nikwambie eh ili umwambie, nikwambie
Ngoja nikwambie ee eh nikwambie kwambie
Nikwambie, nikwambie
Nikwa nikwa nikwambie
Nikwambie, nikwambie
Nikwa

Ukiwa kiziwi, atakuwa bubu
Ukimuhusudu, atakuhusudu
Tenda utendewe (wee)
Tenda utendewe (wee)
Tenda utendewe
Ooh ukiwa kiziwi, atakuwa bubu
Ukimuhusudu, atakuhusudu
Tenda utendewe (wee)
Tenda utendewe (wee)
Tenda utendewe, siri ya peeenzi

Ngoja nikwambie eh ili umwambie, nikwambie
Ngoja nikwambie ee eh nikwambie umwambie
Ngoja nikwambie eh ili umwambie, nikwambie
Ngoja nikwambie ee eh nikwambie umwambie
(Aah haa aahaa) siri ya penzi
(Ou ohh ohoo) kutofichana
(Aah haa aahaa) siri ya penzi
(Ou ohh ohoo) kuaminiana

Ngoja nikwambie eh ili umwambie, nikwambie
Ngoja nikwambie ee eh nikwambie umwambie
Ngoja nikwambie eh ili umwambie, nikwambie
Ngoja nikwambie ee eh nikwambie umwambie

Toa Maoni Hapa

SHIRIKISHA MWINGINE

Your email address will not be published. Required fields are marked *

SHIRIKI KUONGEZA MISTARI