MISTARI YA WIMBO HUU

Utamaduni wangu ni kuuliza why
Why, why, why-why, why
Utamaduni wangu ni kuuliza why
Why, why, why-why, why
Nimekataa kuwa mtumwa, najituma
Hei, he, he, he-he, hee
Kataa kuwa mtumwa, jitume
Hei, he, he, he-he, hee

Form 6, degree hadi masters (sitaki kazi!)
Elimu sio vyeti nachoma (sitaki kazi!)
Wana vyeti mtaani vijana (hawana kazi!)
Natengeneza ajira mtaani, upe kazi

Uko na wasiwasi, mtu bila nafsi
Umeajiriwa shirika la mtu binafsi
Sina wasiwasi, mtu mwenye nafsi
Sijaajiriwa nimeajiri yangu nafsi
Poleni
Mishahara imejaa makato
Biashara mjini ndo zimejaa mapato
Foleni
Ajira itakulinda toa vyeti
Sihitaji kulindwa mi sio mtoto wa geti
Oneni
Kazi ni mpaka wa akili yako
Mpaka ufukuzwe kazi ndo ugundue kipaji chako
Tokeni
Ajira ya mkeo chini ya boss
We ni house girl pekee nchini anakuita boss
Amen
Sivai tai, siikatai
Utamaduni wangu mi ni kuuliza why
Elimu Bongo imekosa plan ya pili
Kosa la pili haufundishwi kuwa tajiri

Utamaduni wangu ni kuuliza why
Why, why, why-why, why
Utamaduni wangu ni kuuliza why
Why, why, why-why, why
Nimekataa kuwa mtumwa, najituma
Hei, he, he, he-he, hee
Kataa kuwa mtumwa, jitume
Hei, he, he, he-he, hee

Form 6, degree hadi masters (sitaki kazi!)
Elimu sio vyeti nachoma (sitaki kazi!)
Wana vyeti mtaani vijana (hawana kazi!)
Natengeneza ajira mtaani, upe kazi

Wanasema hizi single na jingle mzee
Naelekea kuwa bosi kirozay
“Nikki, na binti mzuri nikuozee?”
“Mi bado sipo vizuri nipoozee”
Nakuza network, najuana na watu
Nauza network, naunganisha watu
Nakuza yangu keki, napunguza za watu
Keki, baada ya Mungu ni mzungu
Halafu mimi obvious
Unataka mtoto mwenye akili, serious
Fanya fanya uzae na Nikki Wa Pili, genius
Sitafuti kazi, nataka nitafutwe na wanaotafuta kazi
Kuimba mziki kazi ya Mungu
Sitaki kazi ya mtu, haki ya Mungu
Aah! Kazi ni kipimo cha utu
Amka umekunja sura, kipimo cha mtu

Utamaduni wangu ni kuuliza why
Why, why, why-why, why
Utamaduni wangu ni kuuliza why
Why, why, why-why, why
Nimekataa kuwa mtumwa, najituma
Hei, he, he, he-he, hee
Kataa kuwa mtumwa, jitume
Hei, he, he, he-he, hee

Form 6, degree hadi masters (sitaki kazi!)
Elimu sio vyeti nachoma (sitaki kazi!)
Wana vyeti mtaani vijana (hawana kazi!)
Natengeneza ajira mtaani, upe kazi

Nimekataa kuwa mtumwa, najituma
Hei, he, he, he-he, hee
Kataa kuwa mtumwa, jitume
Hei, he, he, he-he, hee
Nimekataa kuwa mtumwa, najituma
Hei, he, he, he-he, hee
Kataa kuwa mtumwa, jitume
Hei, he, he, he-he, hee

Toa Maoni Hapa

SHIRIKISHA MWINGINE

Your email address will not be published. Required fields are marked *

SHIRIKI KUONGEZA MISTARI