MISTARI YA WIMBO HUU

Siwema, usinipe mateso ya moyo
Na sasa nimechoka kweli nasema ah
Siwema, usinipe mateso ya moyo
Na sasa nimechoka kweli nasema ah
Nilidhani nimepata mpenzi wa kweli
Na kumbe nimepatikana na mambo ya haja kuu
Nia na madhumuni yako nimeshavitambua Siwema kaka
Siwema kaka aa haa haa

Unajitapa mbele ya rafiki zako
Kwamba mimi sina la kusema mbele yako
Umeniweka kwenye kiganja ah haa
Unalotaka, ndilo ninalofanya
Sababu wewe ni mzuri sana
Siwezi kupata mwingine kama wewe
Siwema kaka, unajidanganya

Wema wangu ndio ulionipoonza
Fadhila zote kumbe kwako ni buure
Malipo yake kunifanya mjinga wo woo
Hayo yote ni makosa yangu
Lakini sasa nimejifunza kutokana na makosa
Najiepusha nawe mama ahh!

Nimezunguka Tanzania bara ah
Unguja na Pemba nimefika ah
Nimewaona vijana wenye sifa ah
Wenye kujipamba wakapambika

Nimezunguka Tanzania bara ah
Unguja na Pemba nimefika ah
Nimewaona vijana wenye sifa ah
Wenye kujipamba wakapambika
Kwahiyo nielewe brother..

Sibabaishwi na sura ah
Napenda tabia njema ah
Sibabaishwi na sura yako
Sibabaishwi na sura ah
Napenda tabia njema ah
Usifikiri mimi ni mugeni sana
Ah na sura ah
Napenda tabia njema ah
Nilikupenda kimapenzi
Sibabaishwi na sura ah
Napenda tabia njema ah
Ukaniona mimi sugar mummy lako
Sibabaishwi na sura ah
Napenda tabia njema ah
Tabia njema ndio silaha yako
Sibabaishwi na sura ah
Napenda tabia njema ah
Kila mtu atakupenda kaka
Sibabaishwi na sura ah
Napenda tabia njema ah

Toa Maoni Hapa

SHIRIKISHA MWINGINE

Your email address will not be published. Required fields are marked *

SHIRIKI KUONGEZA MISTARI

VIDEO YA WIMBO HUU