MISTARI YA WIMBO HUU

Shika uliposhikwa ujingapo achia
Maana uliposhika ni muhimu sana kushikilia
Shika uliposhikwa ujingapo achia
Maana uliposhika ni muhimu sana kushikilia

Maneno maneno maneno
Hayashibishi mtu
Maneno maneno maneno
Vita yagombanisha watu
Maneno maneno maneno
Hayashibishi mtu
Maneno maneno maneno
Vita yagombanisha watu

Hizi ni salamu nakupatia Subira
Mi sichokuwepo nitakuwa nasikia
Hizi ni salamu nakupatia Subira mama
Mi sitokuwepo nitakuwa nasikia

Oh oo Subira nisikiize sana
Uendapo mbilini kuna mawifi ujichunge mama
Oh oo Subira nisikiize sana
Uendapo mbilini kuna mawifi ujichunge mama
Acha kusangalai (umpende mumeo)
Acha kusangalai (umtunze mumeo)
Ogopa sana (kovu la ndui halifutiki)
Hayana maana (maneno maneno ya wanafiki)
Ogopa sana (kovu la ndui halifutiki)
Hayana maana (maneno maneno ya wanafiki)

Maneno maneno maneno
Hayashibishi mtu
Maneno maneno maneno
Vita yagombanisha watu
Maneno maneno maneno
Hayashibishi mtu
Maneno maneno maneno
Vita yagombanisha watu

Mambo ya zamani tofauti na sasa mwenzangu
Na siri za ndani zitunze kifuani mwenzangu
Mambo ya zamani tofauti na sasa mwenzangu
Na siri za ndani zisiwafikie walimwengu

Aa chunga mdomo unajidanganya
Unachoweza kufanya kuna wenzako wanaweza fanya
Shoga eh kumbuka siku hizi wanaume wachache
Akienda bafuni akienda kazini akuage shoga eh
Aa chunga mdomo unajidanganya
Unachoweza kufanya kuna wenzako wanaweza fanya
Aa ah hiyo nafasi usiitake uiache utachekwa wee
Wenzio wamaliza stori kwa waganga waipate
Aa chunga mdomo unajidanganya
Unachoweza kufanya kuna wenzako wanaweza fanya

Hehehe ya maji ya ugali hayaonjwi mwenzangu eh
We mwana mwana mwanangu eh

Utaniacha hoi
Hoi hoi
Hata nikikuona sauti sitoi
Utaniacha hoi
Hoi hoi
Hata nikikuona sauti sitoi

Shoga eh kumbuka wanaume siku hizi wachache
Akienda bafuni akienda kazini akuage
Shoga eeh
Aa chunga mdomo unajidanganya
Unachoweza kufanya kuna wenzako wanaweza fanya

We Shirko we jamani we Shirko wewe
Shughuli imeambatana na mvua hii babu
Wanyama wanakula wima
Chezea aa haa neno la kishujaa babu
Vita ifanyike ila raisi nisiuwawe

Aa chunga mdomo unajidanganya
Unachoweza kufanya kuna wenzako wanaweza fanya

Utaniacha hoi
Hoi hoi
Hata nikikuona sauti sitoi
Utaniacha hoi
Hoi hoi
Hata nikikuona sauti sitoi

Toa Maoni Hapa

SHIRIKISHA MWINGINE

Your email address will not be published. Required fields are marked *

SHIRIKI KUONGEZA MISTARI