MISTARI YA WIMBO HUU

Tabasamu nipate furaha
Usiwe unanuna baby, usiwe unauchuna wewe
Tabasamu nipate furaha
Usiwe unanuna baby, usiwe unauchuna wewe

Game kushuka na kupanda
Jana tumeshuka, cheki leo tumepanda
Tumepata idea ya kusambaza kanda
Nimepata shows za Kenya na Uganda
Burundi na Rwanda
Twende pamoja twende tukasake chanda
Mungu akijalia wanazuia kibanda, namiliki kiwanda
Tuko pamoja si ungefunga mkanda
Yote kwa sababu, nipe tabasamu
Tumechoka mitabu hii ndo time ya vitamu
Unapendaga club, unamkumbusha Lam
After two weeks turudi Dar Es Salaam
Tumetesa sana baby (sana, sana)
Vibaya ukinikana baby
Kuniona sina maana baby
Baby, toka mchana alfajiri
Chini utajiri, fake mpaka real
Mapen zi sio siri
Au kwa kuwa tuko wawili, mapenzi ndo ukaona siri?
Kama mabaya yanasemwa kila siku, daily
Wazushi nao hawaishi bifu
Maisha sio kutesa kila siku
Japo pesa ndo kila kitu

Tabasamu nipate furaha
Usiwe unanuna baby, usiwe unauchuna wewe
Tabasamu nipate furaha
Usiwe unanuna baby, usiwe unauchuna wewe

Cheka kidogo ni wewe baby
Nione tabasamu lako girl
Mi naridhika, nafarijika
Ukinuna utaniumiza roho
Cheka kidogo ni wewe baby, oh
Mi naridhika, nafarijika, yeah
Tabasamu, tabasamu
Baby, baby

I say weka amazing smile wacha mi nisebenze
Achana na hao wanaosubiri niteleze
Boogie nami superstar tingisha hizo wezere
(Wezere) wezere, (wezere) wezere
Wakibana Bongo twenzetu kwa Madebe
Twende club zao twende tukaruke debe
Sikia hisia zao sio hisia ka za Reggae
Nawapiga bao wakijirudi kama Chege
Achana na wanga, wanga zao ni kutaga
Mitaa ya Upanga kule wanauza burger
Wanacheza Charanga, unacheza Ragga
Hisia za kimanga, sina hisia za kichaga
Basi baby si ungecheka kidogo
Hujui smile lako linaua mpaka vigogo
Halafu huko nature wala hutumii mkorogo
Pande za Masaki mpaka pande za Kigogo
Wamekutaka hawajakupata hata kidogo
Wakina Roma K, Abuu na Shebi Chogo
Hawajakupata hata kidogo
Haja-haja-hauja…
Blue vipi, mbona sikusikii tena?
Sikusikii uki-flow, mbona sikusikii usema?
Niko busy na baby jamani nishasema
Niko busy na wife jamani nishasema
Mabaya yanasemwa kila siku
Wazushi nao hamuishi bifu
Maisha sio kutesa kila siku
Japo pesa ndo kila kitu

Tabasamu nipate furaha
Usiwe unanuna baby, usiwe unauchuna wewe
Tabasamu nipate furaha
Usiwe unanuna baby, usiwe unauchuna wewe

Toa Maoni Hapa

SHIRIKISHA MWINGINE

Your email address will not be published. Required fields are marked *

SHIRIKI KUONGEZA MISTARI