MISTARI YA WIMBO HUU

Kumbe ni taxi bubu niliemuhusudu
Akaniganda mithiri ya mdudu kupe
Mchana za njano usiku ana nyeupe
Yaliyomo hayamo lakini nimeona it’s not fair

Kweli usilolijua usiku wa giza
Kipenzi cha moyo leo hii kinaniliza mimi
Hisia nilimpa yeye sababu ya kumuamini
Ni chunusi si baharini hata nchi kavu pia jamani wanathamani
Mwenzenu nkasema labda nionapo picha ya kimwana mi ni hoi
Kumbe sivyo bwana vile nilivyodhani awe wangu wa milele
Hivi ndivyo alivyo kupenda anataka kupendwa anaogopa
Sababu ana mengi maovu asije umbuka

Kumbe taxi bubu mchana namba za njano usiku weka nyeupe
Na mi Tonya nishamuhusudu nae kaniganda ganda mithili ya mdudu kupe

Ni bora ningejua mapema kama maisha yako wewe ni ya viwanjani
Sio ufala ulinizuga sana kwamba wewe huna hizo ni wa getini
Mchana unakuja home mitandio kichwani
Usiku ndo sikuoni
Kumbe mwenzangu mimi kiwanja Kinondoni kwa Macheni hamjui nani!
Usiwaone tu machoni jua kuna wengine mazugoni maofisini
Kumbe nao hao (kuwa nao)
Kumbe nao hao (cheka nao)
Kumbe nao hao

Kumbe taxi bubu mchana namba za njano usiku weka nyeupe
Na mi Tonya nishamuhusudu nae kaniganda ganda mithili ya mdudu kupe
Kumbe taxi bubu mchana namba za njano usiku weka nyeupe
Na mi Tonya nishamuhusudu nae kaniganda ganda mithili ya mdudu kupe

Muamini akuamini umvike madini
Mkale kiapo mpaka mwafukiwa aridhini
Sio kichochoroni kavu kavu mdomoni
Kakudanganya kuwa anaishi getini
Hupatikana hata mitaani ukimwi
Usimuamini kwa kumuona kwa macho

Kumbe taxi bubu mchana namba za njano usiku weka nyeupe
Na mi Tonya nishamuhusudu nae kaniganda ganda mithili ya mdudu kupe
Kumbe taxi bubu mchana namba za njano usiku weka nyeupe
Na mi Tonya nishamuhusudu nae kaniganda ganda mithili ya mdudu kupe

Toa Maoni Hapa

SHIRIKISHA MWINGINE

Your email address will not be published. Required fields are marked *

SHIRIKI KUONGEZA MISTARI