MISTARI YA WIMBO HUU

Wasafi
Aiyo Lizer
Aah aah aah aah
Aah aah aah aah
Wasafi Records
Aah aah aah aah

Kama imeshindikana kunirudia isiwe tabu
Usiuforce moyo kupenda usipostahili
Ya nini kung’ang’ania nishachoka kuwekwa sub
Siwezi ooh na mapenzi nishaghairi
Tena niko tayari vipigwe
Vinumbi kengere kwa sherehe
Kinaghaubagha mbele ya umati tuachane
Na kama hautojali tuite
Waumini mapadre na masheikh
Yaishe labda sa kwa nini tutesane
Kweli we ndo nikupendae
Ila unanipa ghadhabu jina
Tusitoane nyongo
Na kama umenichoka eh
Niache kistarabu jina
Usinipe chongo mie

Mwili umebaki kongoro nyama sina ni mifupa
Naiona domboro kabisa siwezi furukuta
Penzi kiporo limeshachina linanuka
Kuishi kokoro purukushani kutwa kucha

Bora tuachane
Bora tuachane siwezi
Bora tuachane
Yamenishinda mapenzi
Mi naona bora tuachane eeh
Tuachane siwezi
Bora tuachane
Yamenishinda mapenzi

Ni dhahiri kisima kimekauka maji
Ndo maana naona ata sina maana tena
Nilifikiri mi gonjwa langu limepata mponyaji
Umeniongezea homa mwili wote watetema
Mi naona basi labda si ridhiki yangu
Kama hunitaki acha tu niende zangu
Ya nini mishikaki ntatafuta boda yangu
Nijinafasi niipande peke yangu

Mwili umebaki kongoro nyama sina ni mifupa
Naiona domboro kabisa siwezi furukuta
Penzi kiporo limeshachina linanuka
Kuishi kokoro purukushani kutwa kucha

Bora tuachane
Bora tuachane siwezi
Bora tuachane
Yamenishinda mapenzi
Mi naona bora tuachane eeh
Tuachane siwezi
Bora tuachane
Yamenishinda mapenzi

Wasafi Records

Toa Maoni Hapa

SHIRIKISHA MWINGINE

Your email address will not be published. Required fields are marked *

SHIRIKI KUONGEZA MISTARI

VIDEO YA WIMBO HUU