MISTARI YA WIMBO HUU

Mwanga haiui chizuyu usituvalie mawani
Usishangae ukiniona nipo na Jay Moe
Jaffarai, Kev na Mchizi Mox
Kaba koo mabishoo, si umeona kutoka droo
Poteza rap katuni mpaka uniite komandoo
Usiulize mi ni nani, jibu S bila MO
Narudi na Wateule masela ebwana soo
Bado nazidi kubisha hodi tunakinukisha
Bado sauti zidisha, Wateule wakilisha
Ona nini na nena, ona wakali wa vina
Ona tumerudi tena, ona mbishi hakuna
Daka kipaza tangaza, tuma ujumbe sambaza
Huwezi imba we nyamaza, katuni tunakataza
Tumerudi kushangaza cheki tunavyochomoza
Commercial wamepooza, jahazi tunaongoza

Tumerudi tena kuonyesha ni jinsi gani
Tunavyoweza kugani, kwa sasa hata zamani
Wateule tuna thamani, mashairi yetu mizani
Kipofu apewe mboni, si mnatucheki mchezoni?
Walitusaka motoni, tunasonga kileleni
Hatuta sema flani, bendera bado hewani
Tunamtaka mpinzani mshindani aje uwanjani
Mandugu wapo mezani tumepandisha lwani
Msije sema majani, haya ni mambo flani
Tunayofanya kwa fani tuzidi ng’ara uwanjani

Tumerudi tena,
Tumerudi tena
Tumerudi tena, Wateule tumerudi tena
Tumerudi tena,
Tumerudi tena
Tumerudi tena, wazima sisi kabisa

2000 nilianza na P Funk, na ’01 akaja Jay Joe
Na ’02 Bongo Records, sasa tuko ndani ya Ojo
Mawazo, kutoka X Men mpaka Jay Moe
Ndio mimi mimi nilieimba “Mvua na Jua” na “Bishoo”
Au unataka demu, wengine wanaomba majukumu
Wengine wanaomba niimbe mshamba
Usinikumbushe huyu demu
Moe tech, moe flav, moe skills, moe conscious spirits
Kama jibu unalo sema nani wa kushindana na sisi
Hatujavunjika, wambea sasa kinawashuka
Wanashtuka kuona mzuka mfano wa mtu anaefufuka
Au kilema anaenyanyuka, magongo anayatupa
Wanashangaa natembea na miguu ilikatika
Moyo wangu mi siuzi, siugharimu uchumi wa akili
Nimeshachoka kila kwenye 4 nipate 2
Hizi siasa za ujamaa ni za watu wa Asia
Mtaani kuna njaa, washikadau mmeshindwa kufikiria

(Ee ee come again)
Tumerudi tena,
Tumerudi tena
Tumerudi tena, Wateule tumerudi tena
Tumerudi tena,
Tumerudi tena
Tumerudi tena, wazima sisi kabisa

Ni mziki ule ule namaanisha Wateule
Mziki umekomaa, mziki umeenda shule
Machizi tulikuwepo toka tunaimba bure
Sasa imekaa vizuri bado mwendo ule ule
Jaffarai, Ulamaa, pia na Kev
Jay Moe, Mchizi Mox hii ni toka ’97
Bado kwenye game tunafanya tu perfomance
Toka Dar Es Salaam tunawakilisha hadi mtoni
Tumerudi tena sasa Wateule namna hii
Si matani crew zote za Bongo hamtufikii
CV yetu inaonyesha hivi
Kazi zinakubalika sitegemei TV
Jaffarai niko busy, na mawazo ya more jize
Kwa mtu anaeijua Wateule kamuulize
Toka watu kibao, toka tumekata mafao
Hip Hop na Ragga ndo tunataka kushushia kwao

Heyo cheki tunavyofoka, cheki tunavyotoka
Cheki tunavyo– mpaka wanashoboka
Nakaa Tabata sio Yombo Vituka
Utapigwa ngumi, jiwe we ukija kwa pupa
Haya cheki tunavyowatupa, cheki tunavyowashusha
Mamistari kama mvua za masika
Watu wamekusanyika, watu wamevutika
Kuwacheki Wateule wanavyochanika

Mikono juu machizi na masista duu
Counter chini kote mpaka counter juu
Rukeni juu, semeni uuh
Ni Wateule tu mwaka huu
Tukipita mtaani ni kama promotion
Kila mtu atataka atutie machoni
Atutazame usoni, juu mpaka chini
Wateule bado tupo, Dar Salaama, mjini

Tumerudi tena,
Tumerudi tena
Tumerudi tena, Wateule tumerudi tena
Tumerudi tena,
Tumerudi tena
Tumerudi tena, wazima sisi kabisa

Tumerudi tena watoto wote kimya
Dawasali nmerudi tena kuwafundisha

Tunawarusha tokea enzi zile
Chaki mpaka Ragga sasa nini unashangaa?
So acha kuzubaa tumekuja tena
Wateule kuja kuwapondesha
Sasa tumekuja kuwashika
Wenye chuki watanuna mpaka kupasuka
Walifanya visa tukavunjika
Sasa tumeshika tena tumewafika
Hii kweli patashika nguo chanika
Tumerudi tena sikilizia vina
Wateule ati mnangoja lakini tunafunika
Tunafunika, tunafunika, tumerudi tena

Toa Maoni Hapa

SHIRIKISHA MWINGINE

Your email address will not be published. Required fields are marked *

SHIRIKI KUONGEZA MISTARI