MISTARI YA WIMBO HUU

Nimejengwa na tungo kuwaelimisha wasioelewa
Wenye vitambi tumbo na hapa juu ya midundo wanavimbewa
Ufupi nyundo ndo kasoro nilopewa
Ukifumbwa fumbo aliyekufumba hataki we kuelewa
Mpinzani hali mbaya baada ya chapter ya Ufunuo
Chekibob utang’oa miwaya usidatike na mpasuo
Safisha roho mbaya safi ikuvishe nguo
Malaya hukosa bwana mwema maana hupenda kwa mkupuo
Muhaya mtulivu hutunzwa ndizi na senene
Haya maumivu zaidi ya ngumi ya taya giza nene
Hip Hop sikivu huelewi fatilia Sebene
Maujanja supplier ukiya-supply uwe na mapene
Wananiombea uhai (ila) niishi kwa mateso
Nikilewa divai ntafurahi Yesu kuja kesho
Uongo haufai ngono haina pepo
Maradhi hunidai hunikopa mafua nlipe lesso
Yesu sio jibu jibu huwekwa nyuma ya sawasawa
Tambua ujana ni ugonjwa ndo maana utu uzima dawa
Muda wa chai umekwisha huu ndo muda wa kahawa
Ngurumo nasikika nae tibu magonjwa bila dawa

Michano adimu kama wali wa udaku
Nacheza rafu juu ya mdundo yapo shwari mapafu
Kichwa cha kuku huwezi kuhimiri kilemba
Ka zamba na baba Luku asili yangu naipenda
Nawamba fasihi natanda emcee
Juu ya anga mi ni mwanga nina angaza jamii
Sina kungu la usingizi utundu huu ni jadi
Nina chungu brand ka Value namudu kwa ustadi
(Jua) cha mtu ni gharama mwisho wake ni gharama
Namfurahia mwana ajuae nini maana
Maisha ni fujo dunia uwanja wa mapambano
Binadamu kwetu kifo ni hukumu kasome Agano
Uone yaliyomo maono kwa ajili yako
Vipi utaishi baada ya kifo umeshawaza
Mengi yanasibu na tiba inaonekana
Ina maana majaribu bado yanasumbua vilaza
Uoga ndio kifo yo usijihisi una gundu
Kijana muombe Mungu ni zamu ya mwana
Maulana akipanga mtu hapangui
Dunia imejaa wanga wametanda buibui yeah

Siteteleshwi na sitishwi na binadamu yoyote
Sitetereki siyumbiki naweza kuishi popote
Kivyote it’s okay ka ukiniacha nisote
Binti niote peace niokote
Maisha yangu sio gazeti niandike unilipe fine
Nishaondoka bila cheti usilipe nimesha-sign
Sifanyi niwafurahishe nafanya nisihangaike
Sifanyi niwanufaishe nafanya ninufaike
Mi ni neno la uzima ninyweni mpate uhai
Ni vigumu kunizima semeni niwatoe nishai
Usinikope sikopeki kama duka la mangi
Usinikwepe sikwepeki kama nuka ya bangi
Ni mwiko kumhonga demu akitaka anihonge mimi
Utamu anaepata yeye ndo utamu naopata mimi
Life inaandaliwa najifunza kila siku
Hakuna aliyezaliwa anajua kila kitu
Mi ni kaka naangaliwa siropoki ka chiriku
Siti yangu imekaliwa na wenye kuimba michiriku
Harakati nishazianza ku-surrender ni mwiko
Mikakati naweka kwanza kinachofata mishiko

Okay okay
Mapenzi yamegeuka weapon
Mwanamke taka
Mama cry for freedom like Ivonne Chakachaka
Nachoandika ni kwa ajili yako fan sio fame
Cause my hip hop is about who I am
Mizito uniandike mistari fake hawaibebi
Wanasema mtoto wa kike akishapenda hajiwezi
Fanya kweli hapa chapaa ogopa kuvuja shida
Baada ya kufeli kukata tamaa amini sio tiba
Nivuka uliposhindwa watatoa wenyewe
Ushuhuda sipo kwa ubingwa nilipo sina kiwewe
Idea zao hazina vitamini umasikini unawachinja
Hili zao sio la Benjamin Mizengo unaepinda
Babu aliniambia mimi ni zaidi ya tufani
Najilinda kwa salama Jabir akili kichwani
Changu kipaji na ujuzi haupimwi kwa tuzo za pombe
Chupuchupu ndio wangu mchuzi nasukumia matonge
Chonde chonde haki hufichwa siri itafichuka tu
Vidonge vinawasukuma na imani ya Mungu juu
Sio mimi mtukufu wa dini ya nini waumini wanifuate
Umaarufu tu hapa mjini ndo unafanya udate

Leo acha nikeshe booth kicheche akeshe uchi
Usiku apewe ngoma na kesho asepe bush
Sio star ni vipi niupende uzushi
Ninavyoinukisha mitaa utasema na genge la ushuzi
Shtuka mbongo kuwa na ubongo wa future
Wangapi wanatoa hongo na kwenye mchongo wanashushwa
Ukweli unaishi uongo unakufa
Maneno hujengwa kwa maandishi kwa kuwa udongo una nyufa
Nafanya emcees wajichinje wanaponisikia
Wanataka wanipinge huku niwalinde wanapoangamia
Ngoma sikinde wajipinde ntawaachia
Kwenye kilinge watalia kwa mbinde za nadharia
Ipo njia uliyechachawa na zama hizi
Nipo pia sijapagawa na taasisi
Nauza madawa wananiita pharmacist
M-Lab mzawa hakuna wa kuchana kama sisi
Ah Napiga punch kama Judo
Ma-rapper wana simanzi ka nafsi ilokosa mvuto
Washikaji hawana wasi wala mshtuko
Wanajua hata kama akifa Nas Songa yupo

Toa Maoni Hapa

SHIRIKISHA MWINGINE

Your email address will not be published. Required fields are marked *

SHIRIKI KUONGEZA MISTARI