MISTARI YA WIMBO HUU

Kwa pamoja tutazame hapa tulipo
Panatuonyesha picha ya mbali uko tuendako mpenzi
Mengi utasikia yakisemwa usiweke moyoni
Kuteleza inatokea mambo ya ndani usiyaweke hadharani
Kama ndege njoo turuke angani wote
Unishike nikushike ili tuwe wote
Mvua ikinyesha iwe baraka ya penzi letu
Lolote likitokea basi tuanguke na tufe wote

Wengine amani tuliyo nayo kidogo wanaiota hawana tena
Pengine pesa si tatizo vipigo kati yao upendo hakuna
Wengine amani tuliyo nayo kidogo wanaiota hawana tena
pengine pesa si tatizo vipigo kati yao upendo hakuna
Heri yetu sisi tushukuru kwa yote heee
Tushukuru kwa yotee
Heri yetu sisi tushukuru kwa yote heee
Tushukuru kwa yotee

Asiye nipenda hakupendi hata siku moja
Siku tunaachana ndo wanachongoja mpenzi
Asiye nipenda hakupendi hata siku moja
Siku tunaachana ndo wanachongoja mpenzi
Juzi nilikosea nikakukuta unalia machozi
Nilipo kuomba radhi ukaelewa samahani ikaokoa penzi

Wengine amani tuliyo nayo kidogo wanaiota hawana tena
Pengine pesa si tatizo vipigo kati yao upendo hakuna
Wengine amani tuliyo nayo kidogo wanaiota hawana tena
pengine pesa si tatizo vipigo kati yao upendo hakuna
Heri yetu sisi tushukuru kwa yote heee
Tushukuru kwa yotee
Heri yetu sisi tushukuru kwa yote heee
Tushukuru kwa yotee

Ni siku nyingi tumejenga mapenzi imara
Wapo hwapendi wameamua kujenga na hila
Wasilete maneno na vikao wakatukalia
Ikawa sababu yakutufanya na sisi kuyumba

Wengine amani tuliyo nayo kidogo wanaiota hawana tena
Pengine pesa si tatizo vipigo kati yao upendo hakuna
Wengine amani tuliyo nayo kidogo wanaiota hawana tena
pengine pesa si tatizo vipigo kati yao upendo hakuna
Heri yetu sisi tushukuru kwa yote eh
Tushukuru kwa yotee
Heri yetu sisi tushukuru kwa yote eh
Tushukuru kwa yote

Toa Maoni Hapa

SHIRIKISHA MWINGINE

Your email address will not be published. Required fields are marked *

SHIRIKI KUONGEZA MISTARI