MISTARI YA WIMBO HUU

Muda umefika kuamsha hisia
Tuunge mkono tutafute njia
Kila kona kuna kijana analilia
Anataka hela bila kuhangaikia
Jielimishe kuwa hiyo haiwezekani
Jiheshimu usisubiri sadaka
Kila siku za wiki mikiki mikiki
Haraka inazaa baraka.
Mzungu Kichaa nayo anahangaika
Ameshazoea maisha ya Kiafrika
Amesoma hadi chuo na masomo ya kitaa
Alikua maskini aliitwa Mzungu Njaa

Twende kazi / vijana
Tutafika mbali sana
Tusiache kazi maana
Bila kazi tutakwenda mrama

Usiwasikilize watu wenye blah blah
Watakupora ulio nayo utabaki na njaa
Kishaa utakuwa unazurua kitaa
Tafuta watu wazuri wanao kufaa
Ukikosa kazi bora ujiajiri
Kila mtu ana kipaji siyo siri
Msafiri kakiri
Sasa ame oa mke wa pili
Usiwe na uwivu na alie na hela
Kumbuka uhuru wa maisha ya kisela
Wengine wana sema
Wenye hela nyingi wanaishi jela

Twende kazi / vijana
Tutafika mbali sana
Tusiache kazi maana
Bila kazi tutakwenda mrama

Unaweza kujiuliza
kama huyu jamaa amekuelimisha
Fanya kazi kutimiza njaa
Usifanye kazi kwasababu ya tamaa
Ukiwa na bahati usimsahau mwenzio
Kumbuka kumwelekeza asiyejiweza
Mfundishe taratibu usiwe na mbio
Naye apate mafanikio
Tugawane umasikini
Tuoteshe uendelevu
Kisha tutahakikisha
Mapato kwa watu wote

Toa Maoni Hapa

SHIRIKISHA MWINGINE

Your email address will not be published. Required fields are marked *

SHIRIKI KUONGEZA MISTARI