MISTARI YA WIMBO HUU

Ulinijaza nami nikajaa
Nikaamini we ndo wangu wa maisha
Ulinilaza njaa ili we usije kosa
Hayo yote we ulijisahaulisha
Uliniaibisha mbele ya marafiki zangu mimi ukawa nao hao hao
Umenidhalilisha, uaminifu wangu mia percent, kwako zero percent
Unanifanya mimi eh, mimi eh, mimi eh, mimi
Ukanifanya mimi eh, mimi eh, mimi eh, mimi
Kwako zero percent

Uzuri wako umenifanya nisilale
Na penzi lako nikaliacha litawale
Afu haukusema uko na mimi, kumbe uko na wale
Unafungisha mechi halafu unasema sare
We mwanamke una roho ya ajabu
Nilikuthamini moyo wako hauna adabu
We ni sista duu, ni bonge la fisadi
Ushanitembeza kwa miguu, kwa uhai miadi
Ki ukweli nimetepeka kwa ajili yako
Umeniweka loud speaker mbele ya shoga zako
Ulipenda visa, sina visa
Kosa sio kosa unajinunisha
Aah kumbe we ni jamvi la matozi
Aah kumbe ulikuwa unanising’ozi
Aah kumbe we ni jamvi la matozi
Aah kumbe ulikuwa unanising’ozi

Ulinijaza nami nikajaa
Nikaamini we ndo wangu wa maisha
Ulinilaza njaa ili we usije kosa
Hayo yote we ulijisahaulisha
Uliniaibisha mbele ya marafiki zangu mimi ukawa nao hao hao
Umenidhalilisha, uaminifu wangu mia percent, kwako zero percent
Unanifanya mimi eh, mimi eh, mimi eh, mimi
Ukanifanya mimi eh, mimi eh, mimi eh, mimi
Kwako zero percent

Unaupeleka mbio moyo kama semi-trailer
Geuza mi poyoyo ukanifunga jela
Penzi lako la kichoyo sina mpya sera
Haya mapenzi ni ushenzi au sina hela?!
Pesa ilikutia kwenye nafsi ya tamaa
Kisha ukatoa penzi moyo umeuachia balaa
We ni bize kwenye simu, mchachu kama ndimu
Umenichenjia kukuona kwa msimu
Hueleweki kama mvua za Dar
Ulitupanga kwa mafungu kama vile dagaa
Ulindatisha mnyamwezi kwa uzuri wako
Ukanfikisha kimapenzi kwa mahaba yako
Aah kumbe we ni jamvi la matozi
Aah kumbe ulikuwa unanising’ozi
Aah kumbe we ni jamvi la matozi
Aah kumbe ulikuwa unanising’ozi

Ulinijaza nami nikajaa
Nikaamini we ndo wangu wa maisha
Ulinilaza njaa ili we usije kosa
Hayo yote we ulijisahaulisha
Uliniaibisha mbele ya marafiki zangu mimi ukawa nao hao hao
Umenidhalilisha, uaminifu wangu mia percent, kwako zero percent
Unanifanya mimi eh, mimi eh, mimi eh, mimi
Ukanifanya mimi eh, mimi eh, mimi eh, mimi
Kwako zero percent

Ili wewe usije kosa
Haya yote we ulijisahaulisha
Mbele ya marafiki zangu mimi ukawa nao hao hao
Umenidhalilisha, uaminifu wangu mia percent, kwako zero percent

Toa Maoni Hapa

SHIRIKISHA MWINGINE

Your email address will not be published. Required fields are marked *

SHIRIKI KUONGEZA MISTARI