MISTARI YA WIMBO HUU

Napandisha bendera hewani kiongozi wa msafara
Kwa imani za kiimani ni amani kama za Vara
Nyimbo za ukombozi ka Bob na Bun B
Sio Mr Blue na mapozi na njozi za Snar Lee
Nahifadhi kumbukumbu mithiri ya chogo la Ongera
Nafanya sipo husudu kwa rhymes sio ngonjera
Mi ni Busta mwenye skills niko faster kwenye beus
Piga ushanta kama Deus kama pastor kwenye njia
Pia ni slim kama Shady here na-scream kama crazy
I got the dreams kama Baby ku-win cash here in a place
Walevi wa mistari waacheni wapepesuke
Mitaani zimajaa habari ka Fid na hisia za Duke
Ukonga is my hood wenyeji wanapaita Gomz
Nasonga nakaza buti ka Escobar ndani ya Bronx
Huna sababu ya kupima mtu mzima na-stay kaya
Kutwa nasaka dhima ka mgosi nisie na himaya
Mi mkali wa freestyle muulize hata Rufunyo
Kote nakubalika nawika toka Lunduno
Naheshimika kwa waumini ka maandiko ya Torati
Mjeshi niko kazini ya nini nivue kombati
Huu sio mziki wa wahindi ni kipindi cha hoja
Mchezoni nitabaki mshindi kwa upeo wa jicho moja
Kutangulia baa kamwe sio kuwahi kulewa
Mtoto kuwahi kukua sio kuwahi kutegemewa
Jipi jajo jipi jajaje
Vipi mayo mi tofauti nawe
Flavour za kuchota pendeza kama nyota
Nateleza kama nyoka ukinigeza we utagota

Sitafsiriki kwa kamusi ka msamiati
Kamwe sikasiriki kwa matusi ka kiuwezo hawanipati
Mwanaharakati mwanahitifaki
Niko moto bati wananivuta mashati kuanguka staki
Sitafsiriki kwa kamusi ka msamiati
Kamwe sikasiriki kwa matusi ka kiuwezo hawanipati
Mwanaharakati mwanahitifaki
Niko moto bati wananivuta mashati kuanguka staki

Niacheni nichane blazameni jikane
Mi ni solid kama ground we ni gas kama methane
Usitake tushindane tena tusibishane
Baada ya saba nane mfiwa mme ni mjane
Tega sikio usikilize next de playa
Ujio unaleta ufagio Mbishi is the best player
Mi ni Zulu kama Shaka lakini sio Bamboo
Mwenyezi shusha baraka Pasaka npate nafuu
Tupo pamoja ka Bushoke na Makore
Na-cross tu ba border we usichoke mi niko dole
Sivukwi ka daraja mithiri ya mto Ide
Naitafuta faraja na upendo utadhani Jide
Nipe heshima usinidharau sababu mi na hasira
Mfano Mina na Mau Hip Hop kwangu ni ajira
We ni Honda mi ni Prado
We ni konda ka Lusajo
Maisha ya ghetto bado ni msoto kama Narajo
Naithamini rangi nyeusi kama Emaerekei
Mi jasusi kama mbuzi since Pac in the days
Bado napiga hatua japo stack on my way
Wanaozingua nawajua here I’m ** the game
We ukileta karateka mi napiga kung fu
Kisha kando nakucheka fake presha iko juu
Maujanja nawapa homa mi natesa mjukuu
Ka enzi za Oliva Ngoma na Allan Kunkuu
Mi ni nunda ka Daz nadunda kama kazi
We unayumba kama basi kwa ndumba unavunja nazi
Hii si Rhumba hii sio Jazz
Na mitumba ndo mavazi
Sio kasumba za wachumba sa mzazi namwaga radhi

Sitafsiriki kwa kamusi ka msamiati
Kamwe sikasiriki kwa matusi ka kiuwezo hawanipati
Mwanaharakati mwanahitifaki
Niko moto bati wananivuta mashati kuanguka staki
Sitafsiriki kwa kamusi ka msamiati
Kamwe sikasiriki kwa matusi ka kiuwezo hawanipati
Mwanaharakati mwanahitifaki
Niko moto bati wananivuta mashati kuanguka staki
Sitafsiriki kwa kamusi ka msamiati
Kamwe sikasiriki kwa matusi ka kiuwezo hawanipati
Mwanaharakati mwanahitifaki
Niko moto bati wananivuta mashati kuanguka staki
Sitafsiriki kwa kamusi ka msamiati
Kamwe sikasiriki kwa matusi ka kiuwezo hawanipati
Mwanaharakati mwanahitifaki
Niko moto bati wananivuta mashati kuanguka staki

Toa Maoni Hapa

SHIRIKISHA MWINGINE

Your email address will not be published. Required fields are marked *

SHIRIKI KUONGEZA MISTARI