MISTARI YA WIMBO HUU

Ukiwa fukara kamwe huwezi kuwa kiburi
Askini jeuri ni msemo tu usiuweke kweli akili
Mwanaume kuwa tajiri ni kama demu kuwa mzuri
Demu wako akiwa kwenye kioo we piga simu tafuta dili
Hela hazilali so ukilala wewe tu
Na zina kasi ya kutengezwa hazikungoji uamke mkuu
Mi na’make money mchana
Na’make money usiku
Iwe kwa tai au kwa jeans mi naingiza mkwanja babu
Naingiza mkwanja na jua na na giza totoro
Mwenzangu saa unazibagua mi sina nazo mgogoro
Begi mgongoni na ramani kama mzungu
Kabla hujafika nilipo nshafahamu my next move
Pesa ni rock mi ni rollwana wa long time ago
Hamuwezi kutuachanisha waliojaribu wote wame’fall
Mikuki imepotea farasi wanarudi wenyewe
Waliowapanda wakati wa kwenda wanaomba wafufuliwe

Usinipigie makofi utachoka mikono itauma plus utamiss nyingine
Unanijua unaniskia
Usinipigie makofi utachoka mikono itauma plus utamiss nyingine
Unanijua unaniskia
Punchlines zinafuatana
Unanijua unaniskia
Punchlines zinaongozana
Unanijua unaniskia
Punchlines zimegandana
Unanijua unaniskia
So usinipigie makofi utachoka mikono itauma

Inakera kujua majibu na watu hawaulizi kitu
We unajua si hatujui ila kaa navyo viote kutu
Maisha ni kama ubao ila hayaandikwi kwa chaki
Siwezi kupa silaha zote nikikupa kwangu zimebaki
Mi ni limited edition nna mission kabla ya kudanja
Ya kwanza kuwa na mkwanja na ya pili kuwa na mkwanja
Namuweka mungu kwanza dunia inashindwa nivunja
Nusu haramu nusu halali upande sheikh na upande ninja
Kila bosi ana bosi wake
Kama mnyonge na mnyonge wake
Mola alikupa punje na punje kawapa wengine
Hakutaka unyanyaswe wala unyanyase watu wake
Alichokupa mi hakunipa ni vyetu tutumie sote
Ukipata nusu ina maana umekosa nusu
Na tuseme anayo mpoki au masanja we haikuhusu
Ni siku ya kwanza ya maisha yangu yaliyobaki
Hivi ndio nnavyotaka iende huu wimbo ni manuscript

Usinipigie makofi utachoka mikono itauma plus utamiss nyingine
Unanijua unaniskia
Usinipigie makofi utachoka mikono itauma plus utamiss nyingine
Unanijua unaniskia
Punchlines zinafuatana
Unanijua unaniskia
Punchlines zinaongozana
Unanijua unaniskia
Punchlines zimegandana
Unanijua unaniskia
So usinipigie makofi utachoka mikono itauma

Sina mjadala na ujinga sina nafasi ya kuuweka
Umri unasonga sina muda mvi zinasogea zitafika
Sipunguziki mimi ka bei za supermarket
Tuna uzito tofauti kama wa shuka na blanket
Naisafisha sabuni ndio inisafishe maungoni
So usininyooshee kidole we ni mchafu zaidi ya mimi
Wenzako hawaombi wanashukuru wanapenda walichopata
Omba samaki upewe nyoka omba upewe usichotaka

Usinipigie makofi utachoka mikono itauma plus utamiss nyingine
Unanijua unaniskia
Usinipigie makofi utachoka mikono itauma plus utamiss nyingine
Unanijua unaniskia
Punchlines zinafuatana
Unanijua unaniskia
Punchlines zinaongozana
Unanijua unaniskia
Punchlines zimegandana
Unanijua unaniskia
So usinipigie makofi utachoka mikono itauma

Yeah
Tumekubaliana kwamba inaisha hivi hivi leo
Haina outro haina nini
It’s yo boy 007 James Bond
Na Hermy B
Of coz
It’s that boy MwanaFA
The mastermind himself
B Hits
We out yo
Peace

Toa Maoni Hapa

SHIRIKISHA MWINGINE

Your email address will not be published. Required fields are marked *

SHIRIKI KUONGEZA MISTARI