MISTARI YA WIMBO HUU

Ogopa matapeli nyumba hii haiuzwi
Moja ya nembo maarufu hapa mjini mzazi
Wote tunataka utajiri so zinatungwa mitkas
Watu wanalia kila siku ka matarumbeta ya arusi
Jua limeshushwa zaidi mjini
Na huwaka zaidi mifukoni
Kila Malaya ana story na zote huwa hazifanani
Kumbuka Zubeda Yule binti wa Professor
Akashindwa jua atamsaidiaje mjini kuna mengi brother
Wanachapa mpaka ndala kwenye nyumba za ibada
Sio wote wana pa kulala usidanganywe na runinga
Huku huku kwenye ufisadi waliopo hawataki kurudi
Hata mbunge wa kwenu yupo huko atakuja uchaguzi
Sio wote mambo ni safi wengine wamegomewa na maisha
Wanaona haya watarudije na story walizowahisha
Hakuna shamba hakuna mbuga labda kuwaibia wajinga
Mawazo yatayofanikiwa ni moja ya kumi ya unayoyafuga
So they say

Yafaa uskize nnayosema
Huku kugumu unaweza kupotea
Na na na na na na (usije mjini)
Na na na na na na (nishakwambia usije mjini)
Eeeeeh eeeh (usije mjini)
Eeeeeh eeeh (nishasema usije mjini)
Eeeeeh eeeh (usije mjini)
Eeeeeh eeeh (narudia tena usije mjini)

Maisha ya huku ni mbinde
Yafaa kutumia akili ya kuzaliwa ndio ushinde
Watu wanahustle everyday
Wapunguze makali ya maisha day after day
Kuna wivu, chuki, ghasia, fitina
Watu wako mbio mbio kupoteza muda hakuna
Wanatoroka na wake hata waume wa wenzao
Wengine hawatosheki wanawachapa mpaka watoto zao
Mbwebwe nyingi vyeti feki wengine wakikopa hawalipi
Na si wote wanaosmile ukadhani wako happy
Hawamaanishi ila ubishi
Maisha hayana hata urafiki
Bora bush town uzushi huko undugu huku cash
Town nani hana deni
Kama hauna kazi muda nao hauendi
Na si kila aliye town basi mjanja
Unaweza kuukamata mkwanja
kisha ukaonekana mshamba
Usije mjini son

Yafaa uskize nnayosema
Huku kugumu unaweza kupotea
Na na na na na na (usije mjini)
Na na na na na na (nishakwambia usije mjini)
Eeeeeh eeeh (usije mjini)
Eeeeeh eeeh (nishasema usije mjini)
Eeeeeh eeeh (usije mjini)
Eeeeeh eeeh (narudia tena usije mjini).

Daisaama samba m’magai
Kama mbwai mbwai
Kuni ni watu jua ndio moto sikutishi mji haufai
Wamasai hawachungi ng’ombe huku wanalinda magari
Washaiba deal ya wamakonde mji ulivyokuwa nishai
Siku hizi hawawindi simba wanasuka dada zetu tu
Mjini huwezi kuwa mtu kama huna deal ya mkwanja mkuu
Nafuu huko kuna waganga kweli
Huku hata dini ni dili
Na kuna manyoya cuz mjini sio kuzuri
Na si kila alie town basi mjanja
Unaweza ukaukamata mkwanja halafu ukaonekana mshamba

Toa Maoni Hapa

SHIRIKISHA MWINGINE

Your email address will not be published. Required fields are marked *

SHIRIKI KUONGEZA MISTARI

VIDEO YA WIMBO HUU

Usije mjini ay ft FA