MISTARI YA WIMBO HUU

 

Christian Bella asubuhi imefika
Saa kumi na mbili jogoo ameshawika kokoliko kokoo
Kokoliko wowo yawee
Wafanyakazi wanaenda maofisini
Wauza sokoni wanaenda soko kuuza
Watoto wa shuleni nao wameshapendeza
Wanaenda shuleni kutengeneza maisha ya kesho

Wafanyabiashara wanaenda biasharani
Wajanja mitaani wanasukuma mikokoteni

Mimi maskini niende wapi
Nianze wapi nitamalizia wapi
Kazi sina deal yoyote mimi sina (kaza moyo)
Natoka asubuhi narudi usiku bila kitu we
Apechalala ndefu mifukoni every day

Sisi masikini twende wapi
Tuanze wapi tutamalizia wapi
Kazi hatuna deal yoyote sisi hatuna
Waliopata kwani walishika kazi ya Mungu
Mola Baba sikia kilio chetu

Tabu na shida kila siku mimi (mimi)
Tabasamu lini utanipitia jamani (jamani)
Maisha yangu kila siku kulia

(Bella sikia)
Mitihani ni mingi usivunjike moyo
Matatizo yana mwisho wake
Oh yeah kwanini we hujiamini
Kama Musa alivuka bahari kwa fimbo na imani
Wewe ni nani
Hata kama wanasema zamani ulikuwa nyani
Oh eh jiamini lelee

Aaa haa aah (usilie)
Aaa haa aah (kaza moyo)
Aaa haa aah (usilie)
Aaa haa aah (kaza moyo)
Aaa haa aah (usilie)
Aaa haa aah

Najiuliza sana (sana)
Kwani mimi Bella hapa duniani
Nilikuja kusindikiza tu wenzangu (jikaze Bella)
Wale tulisoma nao (nao)
Tulikuwa nao wanaishi vizuri na familia zao
Kosa langu ni nini nisilosamehewa
Mola Baba nionyeshe hata ndotoni
Mnasali kwa lugha gani
Nielekee wapi
Kama dini nimeshabadilisha mpaka basi
Naona kama maombi hayafiki kwa Mungu baba
Waliopata kwani walisalimiana na Mungu

Aaa haa aah (usilie)
Na mimi sintokata tamaa (kaza moyo)
Najua kuna siku nitapata (ni kweli)
Ugumu wa maisha ni kipimo cha akili (cha akili)
Christian Bella analia (analia)
Alle Mapigo analia (analia)

Aaa haa aah (usilie)
Aaa haa aah (kaza moyo)
Aaa haa aah (usilie)
Aaa haa aah (kaza moyo)

Christian Bella usilie
Usilie mpaka Mapigo akusikie
Hapo ulipo we usiumie
Usiumie kila mtu mpaka akusikie
Mwanamume analia kama simba
Ndani ya moyo peke yake usiku wa manane
Manane manane sio saa nane mchana

Toa Maoni Hapa

SHIRIKISHA MWINGINE

Your email address will not be published. Required fields are marked *

SHIRIKI KUONGEZA MISTARI

VIDEO YA WIMBO HUU