MISTARI YA WIMBO HUU

Usinihukumu
Kwa makosa ya wako wa zamani
Sio mimi
Niliyesababisha maumivu moyoni
Kama unajiskia
Nihukumu nami nitavumilia
Ingawa naumia
Ila kwako mpenzi nitasubiria
Hatuko sawa
Mbona unanifananisha nae
Unanikosea
Kunivisha makosa yake
Unanifanya najutia
Uamuzi wa mapenzi nilochukua
Hukumuni najitoa
Nilishajua alikukosea

Shori  shori
Nieleze nieleze
Shori  shori
Nieleze nieleze
Mbona unanifananisha  naye
Nami siko kama yeye
Mbona  unanifananisha  naye
Nami siko kama yeye

Moyo wangu ulimchagua yeye
Nilimuamini kupita wengine
Sikudhani kama angenitesa yeye
Sikudhani kama angeenda kwa mwingine
Natamani kukupenda (natamani kukupenda)
Lakini nitaumia (nadhani nitaumia)
Naogopa utanitenda (ooh yeah)
Nitashindwa kuvumilia
Kwa maumivu alonipa
Hakuwa wangu kumbe alipita
Naogopa kukupenda (naogopa kukupenda)
Nadhani nitaumia (nadhani nitaumia)
Kukupenda wewe moyo wangu unasita
Naogopa kukupenda
Mwishowe nikajutia
Mwishowe nikajutia

Baby baby
Nielewe nielewe
Baby baby
Nielewe nielewe
So kwamba nakufananisha nae
Najua mko tofauti nae
So kwamba nakufananisha nae
Najua mko tofauti nae

Usinihukumu
Mpenzi usinihukumu
Penzi lako la muhimu
Mpenzi usinihukumu

Sitokuhukumu
Honey sitokuhukumu
Sitokuhukumu
Ila moyo unanipa wazimu

Usinihukumu
Mpenzi usinihukumu
Penzi lako la muhimu
Mpenzi usinihukumu

Sitokuhukumu
Honey sitokuhukumu
Sitokuhukumu
Ila moyo unanipa wazimu

Shori  shori
Nieleze nieleze
Shori  shori
Nieleze nieleze
Mbona unanifananisha  naye
Nami siko kama yeye
Mbona  unanifananisha  naye
Nami siko kama yeye

Baby baby
Nielewe nielewe
Baby baby
Nielewe nielewe
Sio kwamba nakufananisha nae
Najua mko tofauti nae
Sio kwamba nakufananisha ne
Najua mko tofauti nae

Toa Maoni Hapa

SHIRIKISHA MWINGINE

Your email address will not be published. Required fields are marked *

SHIRIKI KUONGEZA MISTARI