MISTARI YA WIMBO HUU

Nisumbue sumbue usinikubali haraka haraka mimi ah
Mie sitaki kukuacha love naomba ujiamini ii ih
Hakuna mwingine mi anaen’jali maishani
(Unisumbue sumbue usinikubali haraka)
Ni wewe pekee sintoweza kukuacha honey
(Unisumbue sumbue usinikubali haraka)

Naomba uniweke ndani ya chupa kwako nifike kabisa
Mchumba nichizike nife nizikwe na wewe kabisa
Binadamu mi nafahamu sijakamilika
Niponde kama wadau wa the utamu kila dakika
Nitafurahi kama utanimwaga nikija kwa gia za mkwanja
Nitarudi kujipanga ki-underground kama Alphanga
(Naahidi) kukupa moyo ukinifanya niwe na wivu
Kwa mfano nikituma meseji naomba uchelewe kunijibu
(Na sio lazima) kila sehemu ninayokualika utokee
Au kila simu ninayokupigia ewe malkia uipokee
Nyingine unaweza zichunia hiyo inaweza saidia
Kuniweka roho juu na kunijaza uchungu pia
Tusikutane leo mtaani halafu kesho eti uibuke ghetto
Nizungushe ili nijitoe mwisho wa siku niingie mpeku
Usinikubali haraka sababu utaharibu mapenzi
Nami sitaki kukuacha au tuishie one night stand
Sijakupenda leo tu kwa sababu tumekutana
Nilikupenda long time hadi hii leo nakupenda sana
Nikikutazama napata hisia za kuoa
Sio kukudanganya kisha nikaishia kukoa

Nisumbue sumbue usinikubali haraka haraka mimi ah
Mie sitaki kukuacha love naomba ujiamini ii ih
Hakuna mwingine mi anaen’jali maishani
(Unisumbue sumbue usinikubali haraka)
Ni wewe pekee sintoweza kukuacha honey
(Unisumbue sumbue usinikubali haraka)

Usiniambie rangi uipendayo acha mwenyewe niitafute
(Usitunze) kila zawadi ninayokupa nyingine zitupe
Ili nijifunze napoingia ndani ya duka bei isishuke
(Usijichubue) kwa kuwa wanazusha eti napenda ngozi nyeupe
Niimbie “Usiulize” ya Rado tu mkere Fid Q
Ukiona hainiumizi bado ujue kwako nimefika full
Nimechizika boo sio kama ninapita tu
Sijajipachika kama sticker nimekita kama tattoo
(Kama unanipenda nipende) lakini usinikubali haraka
We ni jangwa mie ni mtende nimekuja kama sadaka
Wote walionikubali haraka hatukudumu tuliachana
Sitaki kuamini n’na zali eti kwa kuwa ninajulikana
Sijakupenda leo tu kwa kuwa tumekutana
Nilikupenda long time hadi hii leo nakupenda sana
Nikikutazama napata hisia za kuoa
Na sio kukudanganya kisha nikaishia kukoa

Nisumbue sumbue usinikubali haraka haraka mimi ah
Mie sitaki kukuacha love naomba ujiamini ii ih
Hakuna mwingine mi anaen’jali maishani
(Unisumbue sumbue usinikubali haraka)
Ni wewe pekee sintoweza kukuacha honey
(Unisumbue sumbue usinikubali haraka)

Toa Maoni Hapa

SHIRIKISHA MWINGINE

Your email address will not be published. Required fields are marked *

SHIRIKI KUONGEZA MISTARI

VIDEO YA WIMBO HUU