MISTARI YA WIMBO HUU

Usione hatari we kuwa nami (nami)
Kuwa nami (nami) dada oh
Usione hatari we kuwa nami (nami)
Kama ni shy basi nikuvute tuka-chill tu ghetto ghetto ghetto ghetto
Basi nikuvute tuka-chill tu ghetto ghetto ghetto uuh

Skia (skia)
Hello beautiful please usiniumize
Kichwani niko timamu sio chizi naomba uniskiize
Nataka kuwa Jimmy nataka kuwa mimi
Sintokuzingua sintokupindua mpenzi jiamini
Naomba nafasi nikupatie kile unachohitaji
Nakupenda kweli wanajua hadi washikaji
Weka mpuni nipe mwanya nimiliki the big chair
Njoo nikuimbie Ifunanya ya P Square
Sina mavumba sina nyumba wala Benz
Usiwa na wasi nipe nafasi nikuenzi
Si-act movie wala drama za mapenzi
Kwa hisia nakuimbia katika tenzi
007 James kazimika
Naulizwa ni wewe najibu YES kwa uhakika
Usione hatari kuwa nami dadaa
Ukinitosa ntakukosa na itakuwa balaa

Usione hatari we kuwa nami (nami)
Kuwa nami (nami) dada oh
Usione hatari we kuwa nami (nami)
Kama ni shy basi nikuvute tuka-chill tu ghetto ghetto ghetto ghetto
Basi nikuvute tuka-chill tu ghetto ghetto ghetto uuh

Check
Wasichana wengi ila nimekuona wewe
Napotoka sikuwa na amani nilikuwa na mweme
Napata kiwewe nielewe siko tungi
Nawaza usiku silala ka nakesha disco vumbi
Stereo rap star sio tatizo
Nataka tatua utata usibaki na viulizo
Siwezi leta sizo hata Kizzo anajua
Kwenye shida na matatizo kitulizo utakuwa
Nahitaji ku-settle maisha ya u-bachelor noma
Ntazunguka jiji zima mwisho nipate na ngoma
Situmii kilevi sivuti ganja na fegi
Usidhani huniwezi nkubali nikuite my baby
Usiwasikiize paka shume eti mi mgumu sana
Hapa utapata mume sio shababi wala bwana
Usione hatari kuwa nami dadaa
Ukinitosa ntakukosa na itakuwa balaa

Usione hatari we kuwa nami (nami)
Kuwa nami (nami) dada oh
Usione hatari we kuwa nami (nami)
Kama ni shy basi nikuvute tuka-chill tu ghetto ghetto ghetto ghetto
Basi nikuvute tuka-chill tu ghetto ghetto ghetto uuh

Jyeah jyeah jyeah
Usione hatari kuwa (nami)
Kuwa (nami) dada dada dada
Usione hatari kuwa (nami)
Kuwa sure
Usione hatari kuwa (nami)
Kuwa (nami) dada dada dada
Ah Usione hatari kuwa (nami)
Kuwa yes yes yoh

Usione hatari we kuwa nami (nami)
Kuwa nami (nami) dada oh
Usione hatari we kuwa nami (nami)
Kama ni shy basi nikuvute tuka-chill tu ghetto ghetto ghetto ghetto
Basi nikuvute tuka-chill tu ghetto ghetto ghetto uuh

Toa Maoni Hapa

SHIRIKISHA MWINGINE

Your email address will not be published. Required fields are marked *

SHIRIKI KUONGEZA MISTARI