MISTARI YA WIMBO HUU

Umepika chakula huli
Huoni chapoa
U mpweke mwenye moyo duni
Twakuita soledad
Kula dada kwani huyo haji
Eti yuko na washikaji
Na akirudi matokeo yake ugomvi hauishi
Uko alipo mbali na upeo wa macho yako
Atafanya baya atakalo bila idhini yako
Unangoja na kusubiri utasubiri sana
Hatokeo kwako machoni hutomuona mwenzio

Uko na rafiki zako
Kwako nyumbani kitako
Mkipeana michapo
Huku mkicheka na vicheko oh
Wawapa habari zako
Jinsi bwana anavyokutenda
Hutojua moyo wake
Kwani ni vigumu kufungua moyo

Usijigambe ye akupenda
Hujui akitoka ni nini afanyalo kwako
We wampenda
Katu usiusemee moyo wa mwenzi wako uh woh

Mmelala ni usiku sana
Usiku wa manane
Akili yake kumbe yamuwaza kimwana mwingine
Milio ya simu na ujumbe mfupi vinazidi kwa sana
Ukimuuliza bwana kulikoni utaambiwa ni story
Nao moyo wako punde unaanza kwenda mbio
Mara usiku akuage kuwa anakwenda kutukio
Muulize wapi pande hatokujibu mwenzio
Mara na siku zingine simu yake iko bize nusu saa

Usijigambe ye akupenda
Hujui akitoka ni nini afanyalo kwako
We wampenda
Katu usiusemee moyo wa mwenzi wako uh woh

Angejali moyo wako asingekuumiza huyo
Angeacha atendayo ili wewe upate faraja ah
Lakini umuulizapo juu yeye hukujia
Hathamini chozi lako
Na wala halijali hilo lako pendo

Usijigambe ye akupenda
Hujui akitoka ni nini afanyalo kwako
We wampenda
Katu usiusemee moyo wa mwenzi wako uh woh

Usijigambe ye akupenda
Hujui akitoka ni nini afanyalo kwako
We wampenda
Katu usiusemee moyo wa mwenzi wako uh woh

Toa Maoni Hapa

SHIRIKISHA MWINGINE

Your email address will not be published. Required fields are marked *

SHIRIKI KUONGEZA MISTARI

VIDEO YA WIMBO HUU