MISTARI YA WIMBO HUU

Miaka minane mmejuana
Vingi mmevitenda yani bila kukosana
Chuki baina yenu bila nafasi kutawala
Wengi wangelidhani kuwa kwako ye ni dada
Ndipo basi ukatujulishana
Machache tuliyanena na mawazo kafanana
Kisha maoni yetu yakashinda yakipatana
Nami nikaanza
Kumshuku yeye
Kweli kwa upana

Usuhuba wenu basi kweli tu ni wa uwongo
Imani chafuka udongo
Kumbe tu rafiki yako ana choyo
Yuanichongoza ovyo
Pengine hamfai kuwa marafiki
Sababu kwenye dhiki acha kusaliti
Usuhuba wa uwongo
Usuhuba wa uwongo

Usuhuba wenu basi kweli tu ni wa uwongo
Imani chafuka udongo
Kumbe tu rafiki yako ana choyo
Yuanichongoza ovyo
Pengine hamfai kuwa marafiki
Sababu kwenye dhiki acha kusaliti
Usuhuba wa uwongo
Usuhuba wa uwongo

Sio maajabu kutambua haya yote
Sababu niliziona alama zote
Tangu tulipatana siku ya kwanza
Simu yuanipigia kila usiku na mchana
Nyumbani watembelea, ukiondoka
Neno la ushawishi likimtoka
Nia za kukacha uaminivu tukachoka
Hofu nikatiwa
Nami bila shaka
Kachangayikiwa
Ningelitaka ningefanya
Chochote ningewaza
Lakini nilikaza moyo
Ingali nilipatwa yani bila onyo
Fumbu tumepewa tukitatua tuko pema
Shida likitupata twafahamu tuko vyema
Nisipojichunga
Nitajikuta chini nikijuta

Usuhuba wenu basi kweli tu ni wa uwongo
Imani chafuka udongo
Kumbe tu rafiki yako ana choyo
Yuanichongoza ovyo
Pengine hamfai kuwa marafiki
Sababu kwenye dhiki acha kusaliti
Usuhuba wa uwongo
Usuhuba wa uwongo

Usuhuba wenu basi kweli tu ni wa uwongo
Imani chafuka udongo
Kumbe tu rafiki yako ana choyo
Yuanichongoza ovyo
Pengine hamfai kuwa marafiki
Sababu kwenye dhiki acha kusaliti
Usuhuba wa uwongo
Usuhuba wa uwongo

Muda mrefu nimekana
Yalotokea kuwa hasa
Najua ni rafiki yako
Jiulize yuafanya nini nyuma yako
Ni wazi kutazama
Uti wenu unazama
Ili nikuelezee
Uhaini nao usiende mbele

Usuhuba wenu basi kweli tu ni wa uwongo
Imani chafuka udongo
Kumbe tu rafiki yako ana choyo
Yuanichongoza ovyo
Pengine hamfai kuwa marafiki
Sababu kwenye dhiki acha kusaliti
Usuhuba wa uwongo
Usuhuba wa uwongo

Usuhuba wenu basi kweli tu ni wa uwongo
Imani chafuka udongo
Kumbe tu rafiki yako ana choyo
Yuanichongoza ovyo
Pengine hamfai kuwa marafiki
Sababu kwenye dhiki acha kusaliti
Usuhuba wa uwongo
Usuhuba wa uwongo

Toa Maoni Hapa

SHIRIKISHA MWINGINE

Your email address will not be published. Required fields are marked *

SHIRIKI KUONGEZA MISTARI