MISTARI YA WIMBO HUU

We mama mkaa ndani
Toka nje usikie
Kutwa we kila siku ndani
Toka basi usikie
Kuna habari inavuma

Vuma vuma vuma
Vuma vuma vuma

Na we kaka Ughaibuni
Rudi Afrika usikie
Wewe miaka yote mbali eeh
Rudi basi usikie
Kuna habari inavuma

Vuma vuma vuma
Vuma vuma vuma

Huko Unguja mawee
Huko Unguja mawee
Kuna mtu kasimama
Kwenye kona ya Jahazi
Anahoji uhalali
Uhalali wa Muungano
Na mwingine kasimama
Juu ya kidau chake
Analilia nchi yake
Analilia Zanzibari eeh
Huko bara nako
Kuna mtu kasimama
Juu ya kaburi lake
Analilia roho yake
Analilia Tanganyika eeh
Vuma vuma vuma

Vuma vuma vuma
Vuma vuma vuma

Safu safu wanapita
Wamejaa kwenye mitaa
Na mabango wameshika
Wanalilia gesi yao
Wanalilia nchi yao
Wanalilia jina lao
Na wengine wanajipanga
Waje wadai mlima wao
Watadai mito yao
Watadai migodi yao
Watadai mbuga zao
Watawaua na wenzao
Kumbe imekwisha
Kumbe imetoweka amani eeh
Kumbe imepita
Kumbe haina hodi vita
Kumbe imefika
Kumbe si demokrasia
Kumbe ni demoghasia
Kumbe si democracy
Kumbe ni democrazy
Demonstration of craziness
Viongozi wanajivunia
Kuwa Watanzania
Wananchi wanavumilia
Kuwa Watanzania

Nchi imetiwa giza
Macho yana kiu ya nuru
Kumbe imekwisha
Kumbe imetoweka amani eeh
Kumbe imepita
Kumbe haina hodi vita
kumbe imefika

We mama mkaa ndani
Toka nje usikie
Kutwa we kila siku ndani
Toka basi usikie
Kuna habari inavuma

Vuma vuma vuma
Vuma vuma vuma

Na we kaka ughaibuni
Rudi Afrika usikie
Wewe miaka yote mbali eeh
Rudi basi usikie
Kuna habari inavuma

Vuma vuma vuma
Vuma vuma vuma

Toa Maoni Hapa

SHIRIKISHA MWINGINE

Your email address will not be published. Required fields are marked *

SHIRIKI KUONGEZA MISTARI

VIDEO YA WIMBO HUU