MISTARI YA WIMBO HUU

Mnakula kunywa na kuvaa siku zinaenda
Vya bure hupenda kupewa wala hamna fikira
Kila upande mna-fit siku zinaenda
Vinywa vimejaa ufitini wanaume kama mabinti

Hivi nini kimewauma
Sikumaanisha wote
Na kama kweli hakikuhusu hakiwezi kuuma
Najua wazi mnaelewa ila mu wabishi
Hamtaki kukubali huu ukweli halisi
Vyovyote itavyokuwa ujumbe wangu mmeupata
Hata mkijifanya hamtaki vyema kuelewa
Fanyeni kazi vijana ili tuijenge nchi
Kamwe msikubali kufananishwa na machangudoa

Mnakula kunywa na kuvaa siku zinaenda
Vya bure hupenda kupewa wala hamna fikira
Kila upande mna-fit siku zinaenda
Vinywa vimejaa ufitini wanaume kama mabinti

Ebwana sema sema sema haki yako Jay Dee
Tembo kuvaa vipusa halali haki yako Zey D
Inakuwa vipi wanaume muwe tegemezi
Japokuwa kweli wamama wanawapeni mapenzi
Mkivishwa magauni na vimini mtachukia
Acheni basi kama hamtaki ya kuambiwa ukweli ukweli

Mnakula kunywa na kuvaa siku zinaenda
Vya bure hupenda kupewa wala hamna fikira
Kila upande mna-fit siku zinaenda
Vinywa vimejaa ufitini wanaume kama mabinti

Ukiwakuta kwenye vikao oh vya pombe
Eti wao wasemaji wanaojua yote
Hawatoi hata senti ya kulipa bili
Ikifika zamu yao huenda msalani
Kwa ukuwadi namba moja wao hupenda
Wanaopenda kuwaliwaza mademu wa wenzao
Shoga zangu hebu leteni magauni tuwavishe
Hijabu tuwafunge na vimini vitopu tuwaazime

Mnakula kunywa na kuvaa siku zinaenda
Vya bure hupenda kupewa wala hamna fikira
Kila upande mna-fit siku zinaenda
Vinywa vimejaa ufitini wanaume kama mabinti

Papii umeona wapi mwanaume kunyweshwa pombe

Jay Dee hivi tangu lini rijali zima likasutwa

Nilishangaa ya jana ati nae kaja kitchen party olala

Mnakula kunywa na kuvaa siku zinaenda
Vya bure hupenda kupewa wala hamna fikira
Kila upande mna-fit siku zinaenda
Vinywa vimejaa ufitini wanaume kama mabinti

Igwe igwe lele lele (igwe lele lele)
Igwe igwe lele lele
Ah ah igwe lele lele
Igwe lele lele
Ah ah igwe lele lele
Lele lele (lele lele)
Ah ah igwe lele lele
(Igwe lele lele)
Igwe igwe lele lele (igwe lele lele)
Igwe yoyo igwe lele lele
Igwe igwe lele lele (igwe lele lele)
Ah ah ah ah igwe lele lele
Lady Jay Dee
Uko Papii Kocha eeh
(Mika Mwamba na Norman Dikaka)

Toa Maoni Hapa

SHIRIKISHA MWINGINE

Your email address will not be published. Required fields are marked *

SHIRIKI KUONGEZA MISTARI