MISTARI YA WIMBO HUU

Tulikutana wawili
Tukapendana wawili
Na sasa twaishi wote
Wenye kusema waseme

Ah
Maneno maneno ya nini
Eh
Choko choko za nini

Najua wengi wanatuchukia
Hawapendi watuone wote
Wanaleta maneno ya ugomvi
Wanataka kututenganisha
Nakupenda wangu laazizi
Na sitopenda niachane nawe
Achana na hao mafitina
Mi ni wako pekee

Ah
Maneno maneno ya nini
Eh
Choko choko za nini

Tulikutana wawili
Tukapendana wawili
Na sasa twaishi wote
Wenye kusema waseme

Ah
Maneno maneno ya nini
Eh
Choko choko za nini

Muda wao mwingi kuchunguza mambo
Kuchunguza maisha ya wenzao
Kuongelewa kawaida yetu
Wivu wao unawasumbua
Umbea wote wanauongea
Na mafumbo wanatutupia
Lengo lao kuwa ni kuvunja
Uhusiano wetu

Ah
Hivi inawauma nini
Eh
Hivi inawahusu nini

Tulikutana wawili
Tukapendana wawili
Na sasa twaishi wote
Wenye kusema waseme

Ah
Maneno maneno ya nini
Eh
Choko choko za nini

Mapenzi ya dhati hapa kwangu unapata
Ziba masikio mpenzi wangu twapendana
Hebu tulia unipe mambo usijali wasemalo

Tulikutana wawili (wawili)
Tukapendana wawili (eh hee)
Na sasa twaishi wote
Wenye kusema waseme

Ah
Maneno maneno ya nini (maneno)
Eh
Choko choko za nini (choko choko)

Tulikutana wawili
Tukapendana wawili
Na sasa twaishi wote
Wenye kusema waseme

Ah
Maneno maneno ya nini
Eh
Choko choko za nini

Toa Maoni Hapa

SHIRIKISHA MWINGINE

Your email address will not be published. Required fields are marked *

SHIRIKI KUONGEZA MISTARI