MISTARI YA WIMBO HUU

Najua, wivu ndo mapenzi
Ila wako umezidi, umezidi sana
Sikia, kelele siziwezi
Acha niseme sina budi, inaniuma sana
Tena una gubu, ukianza kusemaga huchoki
Nanyamaza kama bubu, usijikweze, sikuogopi
Unanuna bila sababu, nilichokosa kipi?
Nakuona wa ajabu, mume upendwe vipi?

Afadhali ya mimi kuliko mwenzangu
Umeninyima amani kipenzi changu
Simu tu ikitumika, inakuwa tatizo
Hukawii kukasirika, hutaki jua nini chanzo

Jirekebishe kipenzi changu, malumbano siwezi
Siwezi, na sijazoea

Jirekebishe kichuna changu, malumbano siwezi
Siwezi, na sijazoea

Wivu wa nini
Ayaiya
Umenipanda kichwani eh
Ayaiya
Wivu wa nini
Ayaiya
Umenipanda kichwani eh
Ayaiya

Wivu wa nini
Ayaiya
Umenipanda kichwani eh
Ayaiya
Wivu wa nini
Ayaiya
Umenipanda kichwani eh
Ayaiya

Nilifunzwa unyagoni, kuishi vyema ndoani
Michezo ya kitandani, niliyofunga ngomani
Licha ya kukuthamini, huoni yangu thamani
Umeshindwa niamini, hata nikiwa kazini
Yananicheza machale, haya unayonitendea
Unanifanya nisilale, nikeshe nafikiria

Unarudigi usiku, ona mi ninavumilia
Sisemagi kitu, ni wapi unatokea?

Wivu wa nini
Ayaiya
Umenipanda kichwani eh
Ayaiya
Wivu wa nini
Ayaiya
Umenipanda kichwani eh
Ayaiya

Wivu wa nini
Ayaiya
Umenipanda kichwani eh
Ayaiya
Wivu wa nini
Ayaiya
Umenipanda kichwani eh
Ayaiya

Lady Kaya, Harmonize baby
Mazuu (Record)

Toa Maoni Hapa

SHIRIKISHA MWINGINE

Your email address will not be published. Required fields are marked *

SHIRIKI KUONGEZA MISTARI