MISTARI YA WIMBO HUU

Wala mi sina hila
Ila nafsi yangu inanituma kusema ya moyoni
Wala sina kisasi
Namshukuru Mola huko nlikotoka na sasa nilipofika
Kitanashati haswa
Natiririsha ngoma
Shukrani pia ziende kwa Ostaz Juma Musoma
Mtanashati haswa
Nakinukisha balaa
Shukrani pia ziende kwa Ostaz Juma Musoma

Kesi zangu mi naziacha Mungu atawasomea
Jasho langu kwenye shamba lao walifanya mbolea
Hawakujali nakotokea, shida zojibebea
Wakanifunga akili, miguu huku inatembea
Mama akasema “mwanangu kaza msuli
Ukitaka kizikwa na watu vua koti la ukiburi”
Dawa ya jeuri, kiburi, mimi sio mzuri
Pesa ndo kivuli na ndo mapenzi kama hujui
Kudai haki yangu kumejenga uadui
Napenda maadui zangu na ndugu siwabagui
Atazika nani, sijui, ntakua nae kesho asubuhi
Nani mwenye upendo wa kweli atanikishuka haupungui?
Bado nasukuma kete, weka na mi niweke
Chomeka nichomeke, ngumi double na teke
Kwenye maseke ya makeke
Mfukoni mambo bado kama Chege wa Temeke
Raa!

Wala mi sina hila
Ila nafsi yangu inanituma kusema ya moyoni
Wala sina kisasi
Namshukuru Mola huko nlikotoka na sasa nilipofika
Kitanashati haswa
Natiririsha ngoma
Shukrani pia ziende kwa Ostaz Juma Musoma
Mtanashati haswa
Nakinukisha balaa
Shukrani pia ziende kwa Ostaz Juma Musoma

Naamua kukaa kimya ila na domo la kaya
Hata we nlokuamini leo unanisema vibaya
Usitoneshe kidonda binadamu kinyonga
Ukitaka kuishi wanavyotaka, hee utakonda
Wapo walio furahi wakasema naenda kuteseka
Kumbe kwangu bora amani hata nikilala kwenye mkeka
Siwezi kukataa nimetoka kwenye njaa
Kama hakuna manufaa siwezi ng’agania Dar
Jasho nililomwaga halijachonga hata kitanda
Watu wanaendesha magari na kumiliki vibanda
Inshaallah, Mungu ndo anapanga
Machungu naya-rewind kwenye mind kama kanda
Nashukuru asubuhi kumekucha kwenye mwanga
Mungu ananilinda ananikinga na majanga
Niongoze safari isiishie njiani
Waje sema maisha yangu bila wao haiwezekani

Wala mi sina hila
Ila nafsi yangu inanituma kusema ya moyoni
Wala sina kisasi
Namshukuru Mola huko nlikotoka na sasa nilipofika
Kitanashati haswa
Natiririsha ngoma
Shukrani pia ziende kwa Ostaz Juma Musoma
Mtanashati haswa
Nakinukisha balaa
Shukrani pia ziende kwa Ostaz Juma Musoma

Mziki kwenye lam nausukuma kama mpira
Kama nafunga kushoto kumbe kulia, ila
Ndege nje ya tundu mlinzi tatu bila
Janjaro bado yupo kama desturi na mila

Right, niko makini kwenye game sintong’oka
Japo kuna wanga wanga wanaotaka kuzima nyota
Kuna wanaodiriki hata fala mi kuniita
Ili mradi nipinde wao wabaki wakipeta
Ila nimestuka, siri ndo imefichuka
Mwanzo waliponda fani, na sasa wapo jukwani
Walosema sema ni uhuni wote imewaingia damuni
Wengine bila hayaa, aiyaiya

Wala mi sina hila
Ila nafsi yangu inanituma kusema ya moyoni
Wala sina kisasi
Namshukuru Mola huko nlikotoka na sasa nilipofika
Kitanashati haswa
Natiririsha ngoma
Shukrani pia ziende kwa Ostaz Juma Musoma
Mtanashati haswa
Nakinukisha balaa
Shukrani pia ziende kwa Ostaz Juma Musoma

Oh mama, mama, mama haya maisha
Mai-ma-mamamai ma haya maisha
Oh mama, mama, mama haya maisha
Mai-ma-mamamai ma haya maisha

Toa Maoni Hapa

SHIRIKISHA MWINGINE

Your email address will not be published. Required fields are marked *

SHIRIKI KUONGEZA MISTARI