MISTARI YA WIMBO HUU

(Burn Record)
Na yatakwisha
Mmh aah ee

Ala moja haikai panga mbili nimeamini
Nilidhani nitaweza kuwamudu wote wawili
Ye awepo na we niwe wako
Kwake nipate na we nipate penzi lako
Kweli sitoweza nikuache uende nibaki nilie
Bora kupoteza mali nipate moyo wako nitulie
Kweli sitoweza kuacha uende nibaki nilie
Bora kupoteza vyote nipate moyo wako nitulie

Ulisema umeamua kunisamehe na yatakwisha
Leo tena unataka kunitesa na kuniumiza
Jua kwamba leo mi mwenzio kesho wewe
Haya mateso unayonipa mi mwenzio utapata kwa mwingine

Ulisema umeamua kunisamehe na yatakwisha
Leo tena unataka kunitesa na kuniumiza
Jua kwamba leo mi mwenzio kesho wewe
Haya mateso unayonipa mi mwenzio utapata kwa mwingine

Ukweli wote ulijificha hukuweka wazi
Fadhili zote kumbe bure nani atanienzi
Ningejua pendo lako wala nisingelipokea
Naumia penzi hili sitaweza ku-share

We ndo wa moyoni siwezi ntafanya nini?
Kuishi mbali nawe kwangu nami ni kazi bure
Labda uhai niutoe (niwe chizi nipagawe)
Kama timamu nielewe (naomba unisamehe)
Labda uhai niutoe (niwe chizi nipagawe)
Kama timamu nielewe (naomba unisamehe)

Ulisema umeamua kunisamehe na yatakwisha
Leo tena unataka kunitesa na kuniumiza
Jua kwamba leo mi mwenzio kesho wewe
Haya mateso unayonipa mi mwenzio utapata kwa mwingine

Ulisema umeamua kunisamehe na yatakwisha
Leo tena unataka kunitesa na kuniumiza
Jua kwamba leo mi mwenzio kesho wewe
Haya mateso unayonipa mi mwenzio utapata kwa mwingine

Kwa mwingine kwa mwingine
Uuh (mateso) ooh oo uuh
Clever Sheddy Clever
Clever
Mmh Ben Pol
Linah

Toa Maoni Hapa

SHIRIKISHA MWINGINE

Your email address will not be published. Required fields are marked *

SHIRIKI KUONGEZA MISTARI

VIDEO YA WIMBO HUU