MISTARI YA WIMBO HUU

Yeah
Noma Records
Kalulete
Tamaduni Music Forever
Unajua nini
Rutuba kweli iko kitandani ndo maana ukilala unaota
Yote sawa (Zohan)
Tena ndoto nyingi mpaka zilizoloa sio
Ahh

Tamaduni Music Maybach Music
Since way back mi naplay track ‘move bitch’
Njiwa ana makinda Spika Anna Makinda
Na yeye bado ni spika so anasikika anapoimba
Pedeshee Ndama mtoto wa ng’ombe ndama
Mpaka napagawa kwa drama za hivi zama
Upepo ni kimbunga mchawi ni kimbunga
Oyah nakupungia jamaa na wewe punga
Nash MC P the MC wapo kwenye joint na ipi game hii
Ukienda beach Coco hata Cherie coco
Kuna internation na pia kuna local
Kung fu Master shule headmaster
Ukutani plasta na kidonda plasta
P ni majani chai ni majani
Wanyama na mimea ndio maana hawafanani

Yoh mistari nachana akili nywele nachana
Haina kubishana bwana yote sawa
Sauti zinafana vina vinafanana
Ujuzi unaonekana bwana yote sawa
Mistari nachana akili nywele nachana
Haina kubishana bwana yote sawa
Sauti zinafana vina vinafanana
Ujuzi unaonekana bwana yote sawa

Wasanii wanasanda maiti wana sanda
Wote wanashuka na wengine wanapanda
FM stereo Bboy Stereo
Wanategemeana wakikutana scenerio
Tyson Mike microphone mic
Mmoja bondia mwingine kipaza…right
Mtutu bunduki midundo bunduki
Nyundo juu ya nyundo mafumbo lundo la chuki
Ukionewa kibonde Ephraim Kibonde
Bora kuwa mbabe kuliko kuishi kinyonge
Mapangala Samba Brazil samba
Mbishi anatamba na Sultan Tamba
Kutonya mtonyo pesa mtonyo
Kusonya misonyo pia waziri Sonyo
Wa uhuru mwenge stendi ya mabasi Mwenge
Mwenge mulika stendi ya mwenge wezi wajichenge

Yoh mistari nachana akili nywele nachana
Haina kubishana bwana yote sawa
Sauti zinafana vina vinafanana
Ujuzi unaonekana bwana yote sawa
Mistari nachana akili nywele nachana
Haina kubishana bwana yote sawa
Sauti zinafana vina vinafanana
Ujuzi unaonekana bwana yote sawa

Eyoh
Mayweather boxer nguo ya ndani boxer
Kweli nabaki hoi kama cocacola poster
Jakaya Mrisho Mpoto Mrisho
Ngasa Mrisho mpaka Feruz Mrisho
Bomoa bomoa X hata Samaya X
Picha za ngono X hata mpenzi wa zamani ex
Kigamboni Tungi nikiwapombe tungi
Naongea peke yangu inatoka sauti ya kundi (aah achana na mimi)
Francis Cheka bibi wa Temeke Cheka
Staili ni mateke mapanga makwanja fyeka
‘You Dont Mess With The Zohan’ Nikki Mbishi Zohan
Kila nikirusha track mitaani nabaki sloganyeah
Malcom is like “Hi dad Sitaki pipi nataka uniletee iPad”
Mzazi nadata nabaki “My God Nipe nguvu za Bruce Willis ili ni’Die Hard’”

Eeh Mkuki kwa uchungu kwa binadamu nguruwe
Zohan
Kalulete…Shy-town
Noma Records
Baba Malcom

Toa Maoni Hapa

SHIRIKISHA MWINGINE

Your email address will not be published. Required fields are marked *

SHIRIKI KUONGEZA MISTARI