MISTARI YA WIMBO HUU

Ooh
Hizo ni zama za kale
Ooh
Sangulo na Pepe Kale
Zilipendwa
Eyo Lizer

Eh
Kizamani
Kutoa kadi na maua (zilipendwa)
Wanataka money ukilipa unakwarua (zilipendwa)
Ufundi kitandani sio maguvu kujikamua (zilipendwa)
Unafika ndani hujatomasa unachanua (zilipendwa)
Wanawake wa leo wanataka mikakati
Ukiwa mzugaji haki ya mungu huwapati (zilipendwa)
Mapenzi ya video yatakutoa kamasi
Eti nikinywa maji nakuona kwenye glass (zilipendwa)
Eeh kupiga chabo getto (zilipendwa)
Mkono na dettol (zilipendwa)
Mche na kapeto (zilipendwa)
MA J na Mobeto (zilipendwa)

Ooh
Hizo ni zama za kale
Ooh
Sangulo na Pepe kale
Mhm bolingo ndombolo (zilipendwa)
Twanga Chipolopolo (zilipendwa)
Na maji ya Kandoro (zilipendwa)
Simba wa Morogoro (zilipendwa)

Mtaani sipati sukari guru kabisa (zilipendwa)
Hivi yuko wapi Mb Dogg wa Latifa (zilipendwa)
Babu Tale wapi Papa Misifa (zilipendwa)
Siku hizi party hatuendagi Kibiza (zilipendwa)
Mpira na Pele (zilipendwa)
Tanu na Nyerere (zilipendwa)
Asha Ngedere (zilipendwa)
Aurus Mabele (zilipendwa)
Eti uuze nyumba uweke heshima bar
Eti ulazimishe aliyekukataa
Sabuni kicherema (zilipendwa)
Mabanda ya sinema (zilipendwa)
Lipumba na Mrema (zilipendwa)
Diamond na Wema (zilipendwa)

Ooh
Hizo ni zama za kale (zama za zamani)
Ooh
Sangulo na Pepe Kale (yoyoyo)
Akina Sogi Doggy (zilipendwa)
Chaneli analogi (zilipendwa)
Movie za Saibogi (zilipendwa)
Van Dame Anodi (zilipendwa)

Una nibeep nkupigie umeiweka vocha (haloo)
Ule wewe nilipe mie umeniona lofa
Tena na madada wenye majina acheni visa
Unaitwa ukale diner mnakwenda tisa
Nywele za Kichina (zilipendwa)
Pochi za kuazima (zilipendwa)
Zena na Betina (zilipendwa)
Bashite Gwajima (zilipendwa)

Ooh
Hizo ni zama za kale (zama za zamani)
Ooh
Sangulo na Pepe Kale (yoyoyo)
Mhm Amitabh Bachchan (zilipendwa)
TV kwa jirani (zilipendwa)
Madee Rayvany (zilipendwa)
Zari Ivan (zilipendwa)

Yanini kunichunguza naishi wapi (zilipendwa)
Nala chapati kwa maini au makange (zilipendwa)
Kutwa kunikalia chini una kamati
Oh yarabi masikini kuni dhihaki
Ah Samba Mapangala (zilipendwa)
P Funk Kajala (zilipendwa)
Onyango na Jangala (zilipendwa)
Rufufu Mkandala (zilipendwa)
Vya nini vidomo domo tutupiane tunguli
Kisa pesa za mkopo msimu wa Magufuli
Ah Bongoman Yondo (zilipendwa)
Sikinde Msondo (zilipendwa)
Magari ya Udongo (zilipendwa)
Babu wa Loliondo (zilipendwa)

Ooh
Hizo ni zama za kale (zilivumaga sana)
Ooh
Sangulo na Pepe Kale (yoyoyo)
Ah TV za kichogo (zilipendwa)
Wakina Man Dojo (zilipendwa)
Anti na Iyobo (zilipendwa)
Akina hatupogo (zilipendwa)

Eti msiba ukiona Bundi unataka kupagawa
Tulale makundi makundi kuogopa popo bawa
Zuwena nitampata wapi (zilipendwa)
Zuwena wa zile nyakati eh (zilipendwa)
Kujifanya mapanga zuna wamepinda
Wengine wabeba vyuma na hakuna marinda
Iddi Amini dada (zilipendwa)
Miuno ya H Baba (zilipendwa)
Domo Chai Jaba (zilipendwa)
Michezo ya kibaba baba (zilipendwa)

Wale wapiga madili sasa hali mbaya (zilipendwa)
Hizi zama za Magufuli si za Jakaya (zilipendwa)
Ugomvi wa MrNice na Dudu Baya (zilipendwa)
Vikatuni vya Madenge Baba Ubaya (zilipendwa)
Muhogo Mchungu Mr Bean
Wapi Bambo
Wale wazamiaji wale wa melini
Wazee wa ng’ambo
Hivi yuko wapi Banjamini
Wa Mambo Jambo
Wa Vietnam wa porini
Vita na Rambo
Eh Ndanda Mjelajela (zilipendwa)
Kidali kombolela (zilipendwa)
Max na Zembwela (zilipendwa)
Juma Nature na Fela (zilipendwa)

Ooh
Hizo ni zama za kale (zama za zamani)
Ooh
Sangulo na Pepe Kale (yoyoyo)
Mhm kamanda Daz Nunda (zilipendwa)
Kalumanzila ndumba (zilipendwa)
Simu za Dole gumba (zilipendwa)
Johari na Kanumba (zilipendwa)

Wasafii
Zilipendwa
Zilipendwa
Zilipendwa
Zilipendwa
Ohlilelelilee
Zilipendwa
Wasafi Records

Toa Maoni Hapa

SHIRIKISHA MWINGINE

Your email address will not be published. Required fields are marked *

SHIRIKI KUONGEZA MISTARI

VIDEO YA WIMBO HUU