Majina Kamili : | Juma Kassim |
Lakabu : | Kibla, Kiroboto |
Kuzaliwa : | 21/10/1980 (Umri wa Sasa 43) |
Mji wa Nyumbani : | Temeke, Dar es Salaam |
Mahadhi : | Bongo Fleva, Hip-hop |
Lebo/Studio : | Bongo Records |
Alioshirikiana nao : | Dollo, Wanaume TMK, Wanaume Halisi, Harmorapa, Prof. Jay, K-South, Lady Jay Dee |
Juma Kassim ‘Nature’ (kuz. 21 Oktoba 1980) ni msanii wa muziki wa kizazi kipya kutoka Temeke, Tanzania. Nature, ambaye pia hujulikana kama Kibla ni miongoni mwa wanamuziki wa kwanza wa muziki uliokuja kutambulika kama Bongo Fleva.
Katika kipindi chake cha muziki, amekuwa kiongozi wa makundi kadhaa yaliyotamba ikiwemo Wachuja Nafaka, TMK Wanaume Family na baadae TMK Wanaume Halisi.
Kazi binafsi zilizompatia umaarufu ni pamoja na Hili Game, Kighetogheto, Sitaki Demu na nyingine alizofanya na makundi tajwa aliyofanya nayo kazi.