Ngwair

Wasanii wengine kwa Herufi


Majina Kamili : Albert Mangwea
Lakabu : Cowboy
Kuzaliwa : 16/11/1982 (Umri 31)
Mji wa Nyumbani : Dodoma
Shughuli/Zana : Mwimbaji/Sauti
Mahadhi : Bongo Fleva, Hip-Hop
Lebo/Studio : Bongo Records
Alioshirikiana nao : Chamber Squad, Dark Master, Noorah, Mez B,Lady Jay Dee, TID, Fid Q, Noorah, Mez B, Mirror

Albert Mangwea (16 Novemba 1982 – 28 Mei 2013) maarufu kama Mangwair au Ngwair alikuwa msanii wa muziki wa kizazi kipya nchini Tanzania. Wimbo uliomtambulisha ni Gheto Langu alioutoa mwaka 2000 kwenye studio za Bongo Records.

Albamu yake ya A.K.A Mimi iliyotoka 2003 huchukuliwa kuwa miongoni mwa albamu bora zaidi kwenye muziki wa kizazi kipya nchini Tanzania, ikiwa na nyimbo kama Mikasi, She Got a Gwan, Gheto Langu, Dakika Moja na A.K.A Mimi iliyobeba jina la albamu.

Albamu ya A.K.A Mimi ilishinda tuzo ya Albamu Bora ya Hip-Hop kwenye tuzo za muziki za Kilimanjaro mwaka 2004. Albamu nyingine ya Ngwair ni Nge 1982 iliyotoka mwaka 2009.

Marehemu Mangwea alitambulika pia kwa uwezo wake mkubwa wa kughani mashairi kwa kichwa, maarufu kama ‘mitindo-huru’ moja ya vigezo vya kupima ubora wa wanamuziki kwenye tasnia ya Hip-Hop.

Ngwair alifariki tarehe 28 Mei 2013 nchini Afrika Kusini kutokana na mshtuko wa moyo, ambako hadi kifo chake alikuwa ameshaachia albamu mbili na nyimbo nyingine binafsi na za kushirikishwa.

Toa Maoni Hapa

ngwair kava

MISTARI YA NYIMBO ZAKE

1. Alma
2. BBM
3. CNN
4. Mikasi
10. Kiuno
11. Msela
12. My Baby
13. Action